Tuesday, November 27, 2012

Kukatika kwa nywele








Kukatika kwa nywele
Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.
Mzunguko wa Ukuwaji na Nywele
Mzunguko wa kawaida wa ukuwaji wa nywele hufikia ukomo kati ya miaka miwili mpaka sita na kila nywele hukuwa kwa makadilio ya sentimeta moja kila mwezi. Inakadiliwa kuwa kila mtu hupoteza kiasi cha nywele 20 mpaka 100 kila siku; ingawaje kwa baadhi ya watu hupatwa na hali ya kupoteza nywele nyingi zaidi ya kawaida. Kwa Wanaume au Wanawake upotevu wa nywele si jambo la kufurahisha hata kidogo. Nywele kama Taji la Utukufu wakati wote limempatia mtu uwezo wa kueleza hisia zake kwa njia za mitindo mbalimbali vile impendezavyo. Upotevu wa nywele waweza kuleta mwitiko hasi kwa baadhi yetu na ukosefu wa kujiamini na hata kuleta hisia za muonekano wa umri mkubwa wakati bado wakati.

Zifuatazo ni baadhi ya sababisho ya Upotevu wa Nywele Isivyokawaida.
a) ALOPECIA inaaminika kuwa ni moja ya sababu ya awali na msingi inayoleta upotevu wa nywele mapema kwa wanaume na wanawake. Nywele huwa nyembamba na kusinyaa kisha kukatika, zipo aina mbalimbali za Alopecia.  
b) Upungufu ama hali ya kutokuwepo Uwiano sawia wa vichocheo (Homoni) za kiume ama za kike mwilini zijulikanazo kama; ANDROGENS na ESTROGENS. Mfano wapo wanawake ambao hupoteza nywele nyingi san wakati wa Ujauzito ama mara baada ya kujifungua. Wakati wa ujauzito Uwepo wa kiwango cha juu wa moja wa Homoni waweza kuleta nywele kakatika kwa hali ya kawaida ama isivyokawaida na baada ya kujifungua  nywele huweza kutatika isivyo kawaida kisha Huanza kuota kawaida, katika Hali kama hii hakuna haja ya kutumia Dawa kwa ajili ya kuotesha nywele.
c) Dawa (Medication) baadhi ya madawa yenye kiwango kikubwa cha vitamin A mfano vidonge vya virutubisho, dawa za matibabu ya shinikizo la Damu, Gout, Vidonge vya majira, na Dawa za Msongo wa Akili. Pia matibabu ya kansa na ndiyo maana wagonjwa wengi wa walio katika Matibabu ya Kansa hushindwa kukaa na nywele na kucha wakati wa matibabu.
d) Upotevu wa nywele unatokana kama sehemu ya Dalili ya hali ya kiafya kama Upungufu wa wa Wekundu wa chembe nyekundu za Damu ( Anaemia), Lupus, au KISUKARI ( Diabetes) . Kwa kuwa Upotevu wa nywele waweza kuwa ni Dalili ya awali ya Ugonjwa, hivyo ni muhimu kutafuta sababisho mapema na kutibiwa wa wakati. Kwenye matatizo kama ya Thyroid Gland nywele zaweza kukatika sana.
e) Hali ya Msongo yaweza kuleta hali ya upotevu wa nywele ijapokuwa si kawaida sana hii kutokea
f) Hali ya magonjwa kama Mapunye. Au psoriasis ya kichwani huweza kleta upotevu wa nywele.

Kukatika kwa nywele Matibabu jinsi ya kuandaa mchanganyiko
a. Tengeneza mchanganyiko wa mafuta ya mizeituni (Olive Oil) kiasi katika hali ya uvuguvugu, changanya pamoja mdalasini na Asali kijiko kidogo kimoja kimoja kisha paka kichwani na massage eneo hilo na acha kwa dakika 15-20. Osha na maji Rudia kufanya hivi mara tatu mpaka nne kwa wiki. 
b. Changanya kijiko kidogo kimoja cha Asali na glasi ndogo ya brandy au vodka pamoja na Juice ya kitunguu maji na upake kichani usiku kucha funika na kitambaa au kofia, kesho yake osha na Sabuni vizuri.
c. Pia changanya robo kikombe cha juice ya kitunguu maji na Asali mbichi kisha paka kichwani kwa mtindo wa uchuaji (massage) fanya hivi kila siku usiku.
d.  Fanya uchauji kichwani (Massage) kwa kutumia mchanganyiko wa Asali na kiini cha yai kisha acha kwa muda wa nusu saa kisha osha na maji na sabuni. 

No comments:

Post a Comment


widget