Thursday, June 28, 2012

Kupata Choo Kigumu( constipation)


   Kupata Choo Kigumu(constipation)
Constipation/ hutokea pale ambapo maji mengi hufyonzwa au kama misuli ndani ya utumbo mkubwa inasinyaa taratibu au kiudhaifu nakufanya Choo kupita taratibu kwenye Utumbo mkubwa na hivyo Haja kubwa kupoteza maji mengi kabla ya kufika kwenye Rectum na hivyo kukifanya kuwa kigumu na kikavu isivyo kawaida.

Mambo yanayoweza kuchangia mtu kupata Choo kigumu
Umri: Hali ya kupata choo kigumu/Constipation ni hali inayojitokeza mara nyingi kwa watoto wadogo na watu wenye umri mkubwa ( wazee ) ingawaje pia inaweza kumuathili mtu yeyote. Hii huwapata sana watoto kwa sababu wao hupendelea vyakula vikavu na visivyo na Ufumwele pia watu wazima hasa wengi wasio na meno hupendelea vyakula vilaini ambavyo pia havina Ufumwele wa kutosha.
Hali ya Kiwango cha Uchumi: Watu waishio maisha ya hali ya juu kiuchumi wako kwenye nafasi kubwa sana yakupatwa na tatizo hili kwasababu hawana muda wakula mlo unaofaa, wengi wao hupendelea vikavu mfano chipsi, biscuit nk. ambavyo mwisho wa siku huathili mfumo wa chakula na kusababisha Hali hii.


Aina za Constipation au Hali ya kupata choo kigumu:
·         Hali inayotokea mara moja moja - occasional constipation
·         Hali iliyo komaa-Chronic constipation
·         Hali ijitokezayo wakati wa safari-Travel-related constipation
·         Hali inayojitokeza kutokana na Umri-Age-related constipation
·         Hali inayojitokeza wakati wa ujauzito-Pregnancy-related constipation

Visababishi / causes:
  • Mlo: Moja ya sababu kuba inayosababisha Hali ya kupata choo kigumu ni Ukosefu ama upungufu wa ufumwele katika mlo ambapo hivi hupatikana zaidi katika mbogamboga, matunda, na nafaka zisizo kobolewa pia kwenye cheese, mayai, na nyama. Watu wanao kula chakula chenye Ufumwele wa kutosha wako kwenye nafasi ndogo sana ya kupatwa na Hali hii ya kupata choo kigumu 
  • Kutokunywa maji ya kutosha: Vimiminika kama maji na Juice husaidia kufanya haja kubwa kupita kwenye Utumbo mkubwa kwa ulaini na rahisi, Lakini kuna vimiminika vingine kama Kahawa, coca cola, na vile vilivyo na caffeine huleta mwitikio tofauti na hivyo kusababisha ukavu ama upungufu wa majimaji.
  • Kutokufanya Mazoezi: Uosefu wa mazoezi pia hupelekea mtu kupatwa na tatizo ya kupata choo kigumu. Mfano wa wagonjwa wengi ambao wako vitandani kwa muda mrefu hupatwa na tatizo hili kwa kuwa hawawezi kufanya mazoezi.
  • Madawa: Dawa za maumivu kama (hasahasa narcotics), antacids, antispasmodics, antidepressants, iron supplements, diuretics, na dawa za kifafa husababisha mwendo taratibu wa misuli ya tumbo.
  • Mbadiliko ya Mwili: mfano wakati wa ujauzito, baadhi ya wanawake hupatwa na Hali hii kwa sababu za mabadiliko ya mfumo wa Homoni au wakati mwingine sababu ya uzito wa tumbo ambao hugandamiza matumbo. Juu ya hilo watu wengine hupatwa na shida hii wanapokuwa safarini sababu ya kubadilisha mtindo wao wa milo waliyoizoea kila siku.
  • Matumizi Mabaya ya Madawa ya kulainisha Choo (laxatives) Dawa hizi mara nyingi siyo lazima na ila kwa watu wengine imekuwa ni tabia kuzitumia na Hivyo Mtumizi ya Mtindo huu hufanya Utumbo kuwa tegemezi katika kufanya kazi wake na kwa kufanya hivyo, baada ya kipindi furani mtu hataweza tena kupata choo cha kawaida pasipo kutumia Dawa.
  •  Tabia Hii: Baadhi ya watu huwa na tabia ya kudharau ama kuahilishapale wanapojisikia hali ya kwenda haja kubwa badala yake huwa wanajizuia kwa wakati huo na kwa kufanya hivyo husababisha mtu kupata Choo kigumu Baadaye.  
  • Magonjwa Maalumu: Yapobaadhi ya magonjwa yanayo leta hali hii ambayo ni magonjwa ya mfumo wa viashilia kwa kimombo hujulikana kama neurological disorders, mfumo wa umeng’enyaji chakula,na mingineyo mengi. Matatizo haya hurejesha nyuma mwenendo wa choo kikubwa ndani ya Utumbo mkubwa na mpaka kwenye rectum na Anus. 
  •  Dalili za Hali ya choo kuwa kigumu

No comments:

Post a Comment


widget