Wednesday, July 18, 2012

TIBA YA MAJI / WATER THERAPY

Maradhi ya muda mrefu na mfupi yanasababisha vifo huweza kuponywa kwa urahisi sana kwa njia iitwayo ‘water  therapy’ Utafiti uliofanywa na madaktari wa kijapani na kuchapisha makala juu ya njia hiyo. Na Ikiwa njia hiyo itafuatwa huweza kuponya maradhi yafuatayo:- 
-Kuumwa kichwa, shinikizo la Damu, Upungufu wa Damu, kupooza, mapigo   ya kasi ya moyo na kuzimia.
-Kikohozi, pumu , kifua kikuu.
-Kiungulia, kuharisha damu, kabdhi, bawasili na kisukari.
-Matatizo ya macho.
-Matatizo ya pua, masikio na koo.

JINSI YA UTAYARISHAJI NA UTARATIBU WA TIBA HII YA MAJI.

Baada ya kuamka asubuhi na mapema, kabla ya kupiga mswaki na kunawa uso kunywa bilauri nne za maji, kisha uanapiga mswaki na kunawa uso, baada ya hapo usile wala kunywa kitu chochote mpaka baada ya dakika Arobaini na tano. Taratibu za kufuata; Usinywe maji pale unapomaliza kula chakula kiwe cha usiku, Asubuhi ama hata Mchana, Isipokuwa masaa mawili yapite kila baada ya mlo.
Kwa wale ambao ni wagonjwa hali zao kiafya ni dhaifu wanashauriwa kuanza Utaratibu huu kwa kunywa bilauri moja au mbili za maji na pole pole wanaongeza idadi ya mpaka kufikia bilauri nne. Kwa kweli Kama Mpango huu utafuatwa ipaswavyo basi Itakuwa ya msaada mkubwa sana kwa afya , pia inaonyesha kuwasaidia watu wengi kwa kujenga Afya zao na kuwaponya kwa kipindi kifupi sana.
Tafiti zinaonyesha kuwa Mpango huu unaweza kutibu Maradhi mbalimbali na baadhi ya stadi zimebainisha Muda ambao aina Fulani ya Ugonjwa utaweza kupona kwa kufuata utaratibu huu:- 


Muainisho wa magonjwa na muda wa matibabu:

·         Shinikizo la Damu                                                    --mwezi mmoja
·         Matatizo ya Gesi                                                       --siku kumi
·         Kisukari                                                                     --mwezi mmoja
·         Kufunga choo                                                            --miezi sita
·         Kensa/ salatani                                                         --miezi sita
·         Kifua kikuu                                                                 --miezi mitatu

·         Pia kwa wale wenye gesi na homa ya mifupa dozi ni mara tatu kwa siku. Kwa muda wa siku kumi  tu.
·         Wengine ni mara moja tu kwa siku.
·         Wasioweza kunywa bilauri nne kwa mara moja wanashauriwa  waanze na bilauri moja ama mbili na pole pole wafanye jitihada ya kufikia lengo la bilauri nne kwa siku. Kama ilivyo ada kila jambo mwanzo huwa ni gumu hali kadharika hata Utaratibu huu kwa wale wanaoanza huleta shida kidogo hasa pale mtu anapo kwenda haja ndogo mara kwa mara ila hali hii hurejea kawaida baada ya siku tatu hadi nne hivi.

Zingatia : ni muhimu kufuata ushauri wa kitaalamu kabla ya kuanza matibabu ya aina yeyote mbadala kabla ya kumuona daktari ama kufuata taratibu za kitabibu. Ni vyema kuzingatia hivyo kufika kituo cha Afya kwaajili ya vipimo na ushauri wa kitaalamu.


No comments:

Post a Comment


widget