Mazoezi ya Kegel.
Nini maana ya Kegel ?
Kegel si kitu chochote zaidi ila ni kati majina mengine
mengi maarufu kama Newton’s Law, au Murphy’s law na vivyo hivyo Arnold Kegel ambaye ndiye aliyevumbua
mazoezi haya ya misuli ya sakafu
wa kiuno (pelvic floor muscles) na kuyapa jina lake, ambapo
Arnold Kegel ndiye hasa aliyevumbua faida za maoezi haya mnamo mwaka 1948.
Mazoezi ya Kegel yameonyesha mafanikio makubwa sana
hasa kwa wagonjwa wenye tatizo lakutokwa na haja ndogo pasipo uwezo wa kujizuia
na pia wajawazito wenye shida hii pia, Zoezi hili ni Rahisi sana na huenda huwa
tunalifanya wakati wote na kila siku maishani labda tu ni kwasababu hatufahamu nini
tukifanyacho na faida zake, basi bila shaka punde si punde nitakufahamisha nini
na ni jinsi gani ya kufanya zoezi la Kegel, ambalo kimsingi husaidia kuimarisha
misuli iliyopo chini ya kibofu cha mkojo ambayo husaidia kuthibiti utokaji wa Mkojo.
Kwa wanaume hali ya kutokwa na mkojo pasipo uwezo wa
kujizuia inaweza kusababishwa na udhaifu wa valvu zitwazo urinary sphinter, overactive
bladder au kibofu kisicho na uwezo wa misuli yake kukaza/kusinyaa (contract),
zoezi la Kegel litakusaidia kuimarisha au kuponya hali hii kabisa.
Kegels ni zoezi ambalo ni rahisi sana kulifanya hasa
pale utakapo bainisha hasa ni misuli gani husika, na njia mojawapo nyepesi ya
kubainisha misuli hii ni wakati ule unapokwenda haja ndogo.
Njia au jinsi gani ya kutambua;
·
Jaribu kuzuia mkojo wakati
umeshaanza kukojoa au kama unatoka kwa kasi punguza kidogo kasi ya utokaji wa haja
ndogo/mkojo.
·
Zingatia kutokukaza misuli
yako ya makalio, miguu, au tumbo na wala usizuie pumzi, wakati wa kufanya
jaribio la kubainisha misuli hii
husika.
·
Endapo utaweza kupunguza kasi
ya kutoka kwa Haja ndogo/mkojo au kuuzuia usitoke, hapo utakuwa umefaulu
kubainisha haswa wapi ilipo misuli husika ifanyayo kazi hii na hii ndiyo
huanyiwa zoezi la Kegel
Baadhi ya watu wamebainisha
misuli hii pale wanapovuta taswira ya kuzuia hewa kutoka kwenye njia ya haja
kubwa na endapo utafanya hivi kwa misuli sahihi basi utapata hisia za kuvutika
kuelekea ndani (pulling sensation) na hapo utaukwa umepata misuli hasa ya kiuno
ipaswayo kufanyiwa zoezi hili, pia ni muhimu kuzingatia kufanya zoezi kwa
misuli husika na wala si vinginevyo. (Some men need biofeedback to help them target the
right muscles.)
Jinsi ya Kufanya Zoezi:
- Kaza misuli hii taratibu na uhesabu taratibu moja mpaka tano.
- Legeza tena Misuli hii taratibu kwa kuhesabu taratibu moja mpaka tano.
- Rudia vivyo hivyo mara kumi 10.
- Fanya Seti Kumi za Zoezi la Kegel mara Tatu kutwa kwa Siku, ikiwa na maana kuwa utafanya mara thelasini kwa siku.
Ukiwa ndiyo unaanza zoezi hili kwa mara ya kwanza
yaweza kuwa rahisi kwako kufanya zoeizi umelala kupunguza ukinzani wa nguvu za
uvutano( gravity) na inaweza kuwa rahisi pia kukaza misuli kwa Muda wa dakika
mbili mpaka tatu tu awali.
Baada ya wiki chache baada ya kuanza zoezi ongeza
muda wa kukaza(contract) misuli taratibu mpaka kufikia hesabu za taratibu
kufikia tano au kumi na ufanye zoezi ukiwa umesimama, maana Kwa kusimama
utaongeza uzito zaidi katika misuli yako ya sakafu ya kwenye kiuno na kufanya
jitihada ya kuimarisha Uthibiti wako wa mkojo na Hali ya kuwahi kufika kileleni mapema. Kumbuka
kutokukaza misuli yako ya makalio, miguu, wala ya tumbo wakati wa kufanya Zoezi
la Kegel.
Ni wakati gani Utaanza uona
Matokeo ya Zoezi la Kegel?
Ili kuona matokeo ya zoezi kwa kila zoezi ualolifanya
kawaida huchukuwa Muda hivyo ni vyena kuwa na uvumilivu, ukiwa unafanya zoezi hili
la Kegel Mara Tatu kutwa kwa siku utaweza kuona matokeo mazuri ndani ya wiki tatu mpaka sita,
lakini kuna baadhi ya watu huona mapema
zaidi. Jitahidi kuweka kumbukumbu kila ufanyapo tendo na hii itakuwa ya msaada
sana kugundua mabadiliko na maendeleo ya zoezi (exercise.)
Kama hujaweza kuona mabadiliko yoyote ndani ya mwezi
mmoja, huenda labda bado hujafanikiwa kubaini hasa aina ya Misuli inayopaswa kufanyiwa
zoezi husika la Kegel na hivyo ni vyema ukawasiliana na Daktari aliyekaribu
nawe au tutumie barua pepe kupitia mydailyvalues
Moja ya Mazoezi yenye faida zaidi ni pale
utakapofanya mara zote na wakati wote. na ili kukusaidia kufanya hivyo jaribu kufuata
dondoo hizi:
- Jiwekee kanuni; fanya zoezi la Kegel wakati huohuo kila siku, mfano zoezi la kwanza ni asubuhi wakati unapiga mswaki na jioni wakati unaangalia taarifa ya Habari.
- Kumbuka faida zake; kama utaendelea na zoezi la Kegel amini litaleta mabadiloko makubwa katika hali ya kuzuia mkojo usitoke wenyewe na kukufanya uweze kujizuia kufika kileleni mapema.(Remember the benefits.)
Asante sn kwa post hii ila nahitaji ushauri zaid... Link iliopo hapo km email haifnguki plz naomba mawasiliano yako utakuwa vyema zaidi
ReplyDelete