Mgolo
au kwa kimombo Hemorrhoids hutokea pale ambapo aina ya mishipa midogo Iitwayo
vein iliyopo eneo la mwisho la Utumbo
mkubwa liitwalo kwa ligha ya kimombo Rectum
Kuvimba ama kujaa. Hali
hii hutokea pale ambapo kani ya mgandamizo inapoongezeka ndani yake, mara
nyingi kwa sababu ya kujikamua sana wakati wa kwenda Haja kubwa, pia huwapata
wajawzito kwasababu ya kani ya mkandamizo ndani iletwayo na Ukubwa wa Tumbo
la uzazi na jinsi linavyoongezeka.
AINA ZA MGOLO
Zipo aina mbili za mgolo ambazo
zimepewa majina yake na kutofautishwa kwa sababu ya maeneo zinapojitokeza na
Dalili zake.
MGOLO WA NDANI (INTERNAL HEMORRHOIDS)
Mgolo wa ndani (Internal haemorrhoids)
hutokea ndani ya kuta za Rectum eneo la Utumbo mkubwa lililopo chini mwisho
kabisa na huwa na mtu huwa hawezi kuzihisi uwepo wake, Mara zote huwa hazileti
maumivu ile uwepo wake utagundua pale ambapo mtu hutokwa na Damu wakati wa kupata Haja kubwa damu hii
huchanganyika na choo kikubwa au mara nyingine hutangulia Damu.
MGOLO WA NJE (EXTERNAL HEMORRHOIDS)
Mgolo wa nje (External haemorrhoids)
hujitokeza chini ya ngozi inayozunguka eneo lakutolea haja kubwa kimombo Anus.
Hizi unaweza kuzishika na hata kuhisi uwepo wake zinapokuwa simejaa na wakati
mwingine husababisha Muwasho ama Maumivu au hata kutokwa na Damu wakati wa
kupata Haja kubwa. Mgolo wa nje hutokea
na Kuleta Maumivu Makali pale ambapo Damu hujaa na kuganda ndani ya mishipa
Midogo itwayo Kimombo Vieins.
Mgolo huambatana na 1.Hali ya Kupata Choo Kigumu kwa kimombo tunaita constipation
na pia hali ya kujikamua Unapokwenda Haja.
2.Ujauzito Pia hupelekea kutokea kwa Mgolo, Hali hizi
husababisha kuongezeka kwa kani ya mkandamizo ndani ya mishipa midogo iliyopo eneo
la Rectum iitwayo kwa lugha ya kimombo Hemorrhoidal Viens na kuifanya ijae na
kuvimba. Visababishi vingine ni kama mfano Magonjwa Sugu ya Ini (Chronic
LiverDisease). Mgolo ni Tatizo lililozoeleka sana kwasasa na linakadiliwa
kutokea kwa zaidi ya nusu ya watu wenye umri wa kati ya miaka 50 Hamsini
DALILI ZA MGOLO
Dalili kubwa ni 1. kutokwa na
Damu katika eneo la Haja kubwa pasipo maumivu yoyote. 2. Kupata Choo
kikubwa chenye Damu 3. Damu kwenye Toilet Paper. 4.
Muwasho eneo
la haja kubwa
na kukufanya ujisikie hali ya kutaka kwenda Haja kubwa Muda wote. Kutokwa Damu
unapokwenda Haja kubwa si jambo la kulichukulia kirahisi au kawaida Hivyo unapopatwa
na dalili hii unashauriwa kwenda kituo cha Afya Kwa Uchunguzi wa kitabibu.
Ijapokuwa Mgolo ni moja ya sababisho kubwa la Kutokwa Damu wakati wa kupata
Haja kubwa kunaweza kuwa bado na visababishi vingine kama Uvimbe, Maambukizi
kwenye njia ya haja kubwa NK.
MGOLO WA NDANI ULIO JITOKEZA
NJE.
Hii hutokea pale ambapo Mgolo wa
ndani Unapovimba sana na kujaa kisha hushuka taratibu kutoka eneo Ulipoanzia
mpaka Kutoka nje ya njia ya haja Kubwa. can be felt as a lump outside the anus;
·
Upo uwezekano wa kuuludisha ndani
taratibu ijapokuwa hii hitakuwa jawabu la kudumu nikiwa na maana kuwa tatizo
laweza kijitokeza tena.
- Mgolo uliotoka nje Unaweza kujaa zaidi kama hautarudishwa kwa wakati.
MGOLO WA NJE ULIOPATWA NA DAMU
KUGANDIA
MGOLO uliotokewa na mgando wa Damu ndani
yake Huleta Maumivu Makali sana.
- Kuganda kwa Damu panapo jitokeza Mgolo Hujaa na kuvimba sana na vimbe hii husababisha kuongezeka kwa maumivu..
- Maumivi makali zaidi wakati wa kupata Haja Kubwa na wakati Mtu amekaa.
- Hali hii ya kuganda kwa Damu ndani ya Mgolo inahitaji Matibabu ya Kitabibu.
WAKATI GANI UMUONE TABIBU
- Pale Utakapoona kutokwa na Damu katika njia ya haja kubwa ijapokuwa kwa Mgolo ni kitu cha kawaida ila hunda kukawa na sababu nyingine zaidi zinazosababisha.
- Pia Uangalizi wa kitabibu na Matibabu ya haraka inapotokea Hali ya kutokwa Damu kwa Mtu anayetumia Dawa za kufanya wepesi wa Damu kitaalamu mfano warfarin (Coumadin), clopidogrel (Plavix), or prasugrel (Effient) nk.
- Mtu aliye na dalili nyingine mfano kichwa kuwa chepesi, kizunguzungu na udhaifu wa mwili huenda akawa amepoteza Damu zaidi na anahitaji Uangalizi wa haraka wa katabibu.
- Mogolo huwa hausababishi maumivu ya Tumbo Lakini Hali hii ikijitokeza uanhitaji kumuona Tabibu mapema iwezekanavyo.
- Mgolo Uliotoka nje ambao umehindikana kurudi ndani hata kwa kuurudisha taratibu unahitaji Uangalizi na Ushauri wa Kitabibu.
- Mgolo wan je Uliopatwa na Mgando wa Damu waweza kuleta amumivu makali yanayohitaji Matibabu ya kitabibu Mapema.
MATIBABU YA MGOLO
Maji ya Uvuguvugu
- Kukalia Maji ya uvuguvugu kutwa Mara Tatu kwa muda wa Dakika 15-20 husaidia kupunguza Mgolo ulio vimba..
- Ni muhimu kukausha vizuri eneo la haja kubwa baada kukalia maji ya uvuguvugu l kuepusha muwasho katika maeneo yanayozunguka eneo hilo.
Badilisha MLO
- Ongeza unywaji wa vimiminika na Ufumwele wa kutosha katika kila Mlo wako hii itakusaidia kupunguza Hali ya kupata Choo Kigumu na hivyo kukusaidia Kupunguza kani ya mgandamizo, kutokwa na Damu na kupunguza kuvimba kwa Mgolo.
·
Vilainishi vya Choo Kikubwa
Vilainishi vya choo kikubwa
husaidia kwa sehemu ijapokuwa choo kilaini sana husababisha vimbe ndani ya njia
ya haja kubwa ama maambukizi. Ivyo ni vyema ukashauriana na Tabibu ama mfamasia
wako.
Mambo ya kuzingatia
- Ni vyema mtu mwenye tatizo la mgolo kutokaa kitako kwa muda mrefu sana
- Mazoezi ni muhimu sana naya msaada mkubwa katika kupunguza Hali ya Kupata Choo Kigumu na hivyo kupunguza Kani ya Mgandamizo ndani ya Hemorrhoidal Veins. Pia ni vizuri mtu kwenda Haja pale unapojisikia kufanya hivyo wala usijicheleweshe.
MTAZAMO JUU YA MADAWA
|
MATIBABU YA KITABIBU
Mgolo wa ndani uliotoka nje. (Prolapsed Internal Hemorrhoids)
- Nyingi ya Migolo ya ndani inayotoka nje Hurudisha ndani kwa kuisukuma taratibu kupitia njia ya haja kubwa.
- Kama Mgolo Utaendelea kubaki ukiwa umevimba na kujaa ukiwa nje ya njia ya haja kubwa na hakuna lakufanya katika hali kama hii njia za Upasuaji hutakiwa ili kuondoa Tatizo.
Mgolo Uliopatwa na Mgando wa Damu. (Thrombosed Hemorrhoids)
·
Mgolo wa nje uliopatwa na Mgando
wa Damu (Thrombosed external haemorrhoids) unaweza kuleta maumivu Makali
yanayoambatana na kitu kigumu katika eneo la haja kubwa na Haiwezekani
kukisukuma ili kingie ndani. Mara nyingi Damu iliyoganda ndani ya Mgolo
inahitaji kuondolewa kitaalamu kupitia Tabibu.
DONDO: Zipo aina ya Dawa ambazo endapo mtu atafuata
Taratibu zinazotolewa hutibu Tatizo hili Moja kwa Moja, Dawa hizi
zimetengenezwa ki-Asilia kutokana na Aina Fulani ya Mimea: Unaweza kuzipata
kupitia Hapa Mydailyvalue
Jina la Dawa: Pilex Ointment and Pilex Tablet
Matumizi: Hutibu 1. Mgolo/ Mjiko ( hemorrhoids)
2. Hali ya Kuvimba Vena za Miguu (varicose veins)
· Upasuaji (Surgery)
Kuna njia nyingi za upasuaji pale
utakapoona Maumivu na kutoka Damu kusikokoma kwa muda Mrefu: kama unahitaji ushauri
kutoka kwa wataalamu wetu ama kumwona Tabibu kwa ushauri na uchunguzi zaidi
wasiliana nasi kupitia mydailyvalue
Jinsi ya
kujikinga usipate Mgolo
Athali za kupatwa na Mgolo unaweza kuzipunguza kwa Kula Mlo
/Chakula chenye Ufumwele wa kutosha, Kunywa Maji ya kutosha, Fanya Mazoezi
Mara kwa Mara, jitahidi kwenda Haja kubwa Pale tu unapojisikia kufanya Hivyo.
No comments:
Post a Comment