Tuesday, November 27, 2012

MDALASINI NA ASALI


MDALASINI NA ASALI
Asali inafahamika vyema Duniani kote Kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee. Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini (cinnamon)  wa kawaida. Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko dawa ya kusisimua iletayo afya bora.
Zipo baadhi ya hali zinaweza kutibika kwa kutumia Asali na mdalasini:

Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya Asali pamoja na sehemu mbili za maji vuguvugu na kijiko kimoja kidogo chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika. Jifunze zaidi hapa:-
Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele. Jifunze zaidi hapa:-

Kipimo cha helemu cha watu waliokuwa na afya nzuri (katika jaribio) kilishuka kwa wastani wa asilimia 10 katika muda pungufu ya masaa mawili baada ya kunywa bilauri moja….. Jifunze zaidi hapa:-
Asali ina historia ndefu ya kuamsha uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi ….. Jifunze zaidi hapa:-
Wawezakufurahia vyakula vyote unavyopenda, kuwa na afya nzuri na kupunguza uzito wa mwili….. Jifunze zaidi hapa:-
6. Ukungu wa miguuni
Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini (vya chai). Pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Kwa kutumia njia hii hali ya ukungu itakwisha kwenye kipindi cha wiki moja endapo utafuata taratibu.
7. Maambukizo kwenye kihofu cha mkojo
Bilauri ya maji vuguvugu yaliyochanganywa na vijiko viwili vya chai vya mdalasini na kijiko kimoja cha chai cha asali huondoa bacteria kwenye kibofu. Unaweza ukatumia juisi ya cranberry badala ya maji ikiwa mambukizo ya kibofu yatakuwa sugu.
8. Maumivu ya jino
Changanya sehemu tano za asali, na sehemu moja ya mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino. Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika kisha kwa muda hadi maumivu yatakapotoweka.
9. Vidonda vitokeavyo baada ya mgonjwa kulala kwa muda mrefu
Saladi ya kupaka vidonda iliyochanganywa na asali pamoja na mdalasini kwenye chai ya raspberry nyekundu ni dawa nzuri ya kuondoa maumivu makali ya canker sores.
10. Mafua                                                                
Mafua yameshaeleweka ya kwamba hupotea/huondoka baada ya masaa machache baada ya waathirika kutumia kijiko kimoja kikubwa cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko (cha chai) cha mdalasini, mchanganyiko huu ni mahususi katika kusaidia kuondoa chafya na kuvimba koo.
11. Mchafuko wa tumbo
Asali imetambuliwa kwa kipindi kirefu kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na hii tiba ya kimaajabu vilevile itapunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo. Kula asali pamoja na mdalasini huweza kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi/acid kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi iliofanywa huko India na Japan.
12. Ugonjwa wa Moyo
Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara-kwa kupakaa wakati wa kifiingua kinywa. Kula asali ya mkate wa ngano yenye nyuzinyuzi nyingi iliyopakwa kijiko kimoja {cha mezani} cha mchanganyiko huo hapo juu kila siku. Tiba hii ya maajabu iliweza kupunguza kuganda kwa mishipa ya damu kwa 74% ya wagonjwa waliokuwa katika nyumba za kutunzia wagonjwa - utafiti mmoja ulionyesha.
13. Shinikizo la damu
Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo ya maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya watafiti wa kitaliano kuwapa dozi za mara kwa mara za asali ilyochanganywa na mdalasini. Vipimo vya shinikizo la damu vilionyesha ukawaida na wote 137 waliofanyiwa jaribio hilo waliripoti kujisikia vyema/vizuri baada ya wiki chache za tiba hii ya ajabu.
14. Kinga ya mwili
Kinga yako ya mwili itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja - wataalamu wanasema. Utafiti wa kitiba unaonyesha kwamba hazina kubwa ya vitamini{vivurutubisho}na madini pamoja na michanganyiko mingine iondoayo magonjwa pamoja na kinga itolewayo na chembechembe nyeupe za damu, husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea virus na bacteria.
15. Kutokuchaguliwa kwa chakula (Digestion)
Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo(kula chakula) huondoa kiungulia na wataalamu wanasema kwamba asali husaidia kutolewa kwa juisi zinazotumika kuchaguliwa kwa vyakula tumboni na mdalasini unaongeza spidi ya kuchaguliwa kwa vyakula.
16. Flu
Tafiti moja ya kihispania imethibitisha kwamba aina ya dawa moja asilia ya ajabu ambayo huharibu virusi (vimelea) viletavyo Homa ya Flu
17. Umri wa kuishi
Unaweza kuishi kufikia hadi miaka 100 na kufurahia maisha ya afya na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai ya mdalasini na asali. Kutengeneza kinywaji hiki kitamu, weka vijiko vine (vikubwa) vya mdalasini katika vikombe vitatu vya maji na koroga kwa dakika 10. kunywa robo kikombe kutwa mara tatu au nne na hivyo utakuwa na kinywaji kingi.
18. Chunusi
Changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi. Uwezo wa asali wa kuua bacteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili.
19. Kuumwa na wadudu (kwa washawasha) wenye sumu
Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati mwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi viuvimbe vinapotoweka kabisa.
.20. Sarakani
Utafiti uliomalizika karibuni huko Australia na Japan, umeonyesha kuwa asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa anayetumia madawa ya kutibu sarakani. Katika tafiti iliyofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua kwa kiwango kikubwa sarakani ya mifupa na tumbo, wale waliokuwa wakitumia kila siku dozi za asali na mdalasini, walionyesha maradufu kupata nafuu kuliko wale waliokuwa wakitumia wakitumia madawa ya sarakani pekee. "Tuliwapa kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi" .anasema Dr Hiroki Owatta. "Wengine waliendelea na milo ya kawaida".
21. Uchovu
Upo ushahidi mpya kwamba sukari asilia zilizopo kwenye asali zina uwezo wa kuongeza nishati mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu, wataalamu wanapendekeza kuchauganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji, nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi. "Kunywa tena saa 9 alasiri wakati nishati {nguvu}inapoanza kushuka" anashauri Dr Milton Abbozza ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa. "katika wiki moja hii itajionyesha".
22. Kuvimba Nyayo
Chua asali na mdalasini vuguvugu katika {miguu} nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu na kazi au baada ya mazoezi marefu. Rudia kila asubuhi halafu nawisha nyayo kwenye maji baridi na vaa viatu.
23.Harufu mbaya kutoka mdomoni
Waamerica wa kusini wanasukutua kwa kutumia asali na mdalasini pamoja na vuguvugu kila asubuhi ili kufanya harufu toka mdomoni kuwa nzuri na safi kiasilia. Katika Asia ya kusini mashariki, watu hula kijiko cha mdalasini na asali ili kuondoa harufu mbaya mdomoni (halitosis). Wataalamu wanaamini kwamba uwezo wa kuua bacteria uliopo kwenye asali ndiyo unaopigana na harufu mbaya itokayo mdomoni.
24. Kupungua kwa usikivu
Dozi za kila siku za asali na mdalasini hufanya hali ya usikivu kuwa makini kama ilivyogunduliwa na Wagiriki wa zamani.

Zingatia: ni muhimu kufuata ushauri wa kitaalamu kabla ya kuanza matibabu ya aina yeyote mbadala kabla ya kumuona daktari ama kufuata taratibu za kitabibu. Ni vyema kuzingatia hivyo kufika kituo cha Afya kwaajili ya vipimo na ushauri wa kitaalamu.




No comments:

Post a Comment


widget