MAELEZO
YA MSINGI KUHUSU KILIMO CHA VITUNGUU Jifunze juu ya Constipation.
Vitunguu ni zao la mbogamboga na hulimwa kwa ajili
ya balbu zake.
Hulimwa nyanda za baridi kwa wingi sana. Nyanda
zenye joto vitunguu
hulimwa pia. Tanzania vitunguu hulimwa sana sehemu
za Mang’ula, Mgeta
na Singida. Hata hivyo vitunguu hustawi
maeneo mengi yaTanzania. Vitunguu
vinaweza kulimwa mwaka mzima
endapo majiyanapatikana. Vitunguu vina
matumizi mengi sana na
vina madinijoto, chuma, vitamin A,
vitamin B, vitamin
C na vitamin E.
Halijoto
Joto linatakiwa sana kwa ajili ya ukuaji wa balbu
ila joto likizidi vitunguu
hukomaa mapema kabla balbu hazijafikia
ukubwaunaostahili, hivyo
mkulima anaweza kupata mazao
kidogo.
UTANGULIZI
Vitunguu maji
hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali
ya hewa ya ubaridi wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za
kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye
nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Nchini Tanzania, vitunguu maji hulimwa kwenye mikoa ya Iringa wilaya ya
Kilolo mpakani mwa mkoa wa Morogoro na kwenye maeneo ya mto Ruaha, mkoani Arusha sehemu za Mang’ora na Babati, Kilimanjaro, na Morogoro wilayani Kilosa sehemu za Lumuma na Malolo na
baadhi ya sehemu za Mkoa wa Singida.
Hali ya Udongo
Vitunguu maji huhitaji udongo wenye rutuba, usiopasuka,
usiotuamisha maji na wenye mboji ya kutosha. Hali ya udongo
katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0.
Hali ya hewa
Hali ya hewa ifaayo ni ile ya ubaridi wastani. Joto
linalohitajika ni
kati ya nyuzi joto 13 hadi 24°C ingawa kwa miche iliyoko
kwenye
kitalu joto zuri
ni la nyuzi 20 hadi 25°C. Joto la juu hufanikisha
utengenezaji wa kitunguu na ukaukaji.
Aina ya Vitunguu maji
Kuna aina nyingi ya vitunguu maji. Aina hizi zinaweza kutofautishwa
kulingana na:
(i) rangi ya ganda
la nje la kitunguu kilichoishavunwa;
(ii) radha (utamu
au ukali) wa kitunguu chenyewe;
(iii) mahitaji ya
mwanga katika uzaaji: kuna aina yenye kuhitaji
siku fupi (mwanga
wa saa 10 hadi 12 kwa siku) na aina
ihitajio siku
ndefu (saa 13 hadi 14 za mwanga kwa siku) ili
kuweza kuweka
kitunguu. Aina ya kwanza ndiyo ilimwayo
katika nchi za
tropic.
Uoteshaji
miche na Upandaji
Vitunguu maji
huoteshwa zaidi kwa kutumia mbegu kwenye kitalu
na kisha
kupandikizwa shambani. Kiasi cha kilo 3.5 cha mbegu hutoa
miche ya kutosha kupandikiza eneo la hekta moja ya shamba.
Kusiha mbegu kwenye kitalu
Mbegu zinasiwa kwenye kitalu kilichoandaliwa vizuri. Mbegu hupandwa kwenye kina cha sentimita moja kwa kumiminwa
polepole kwenye mistari/mifereji iliyoandaliwa vizuri. Kisha mbegu
hufukiwa kwa kunyunyizia udongo juu ya mbegu zilizoko kwenye
mifereji. Mbegu huota baada ya siku 7 hadi 10. Lakini hii hutegemeana
na hali ya hewa. Kwani mbegu huweza kuechelewa kuota hadi mpaka siku 21 udongo unapokuwa wa baridi. Hali ya hewa ikiwa nzuri,
mbegu
uota mapema zaidi, hata ndani ya siku
4.
Kupandikiza
vitunguu shambani
Miche hupandikizwa
inapokuwa na urefu wa sentimita 15 na unene
1/2
au 3/4 ya
penseli kwenye shina. Miche hii huwa imetimiza umri
kati ya wiki 7 hadi 9 kulingana na matunzo. Miche
inapandikizwa
kwenye nafasi ya upana wa sentimita 20 hadi 30 na nafasi
ndani ya
mstari ni
sentimita 10 hadi 15.
Kuandaa
shamba
Kabla ya
kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe
kabisa. Kisha
matuta au majaruba hutengenezwa ili kurahisisha
umwagiliaji.
Mbolea
Vitunguu maji
vinamahitaji makubwa ya rutuba ya udongo. Hukua
vizuri vinapopata
samadi ya kutosha kiasi cha tani 25 hadi 40. Kwa
hekta. Mbolea
isambazwe shambani baada ya kupandikiza, lakini ni
vizuri zaidi kama
ikichanganywa kwenye udongo kabla ya
kupandikiza. Kwa
kuzingatia mazao ya tani 18 kwa hekta, vitunguu
huchukua kutoka
katika udongo, kiasi cha wastani wa kilo 66, 11 na
70 za virutubisho
aina ya Nitrojeni, Fosiforasi na Potasiam.
Hivyo kiasi cha
mbolea kinachopendekezwa ni kilo 450 hadi 565 za
mbolea ya NPK (10-10-20) kwa hekta. Mbolea huwekwa siku 7
hadi
10 kabla ya kupandikiza. Kisha, inapendekezwa kuweka kiasi
cha
kilo 13 hadi 18 za Nitrojeni baada ya wiki tatu hadi nne,
ili kuongeza
ukuaji wa mimea. Upungufu wa kirutubisho cha Nitrojeni
unaharakisha ukomaaji na unapunguza ukubwa wa kitunguu.
Kirutubisho hiki kikizidi kupita kiasi huongeza ukubwa wa
kitunguu
na unene wa shingo ya kitunguu, tabia ambayo upunguza ubora
Umwagiliaji:
Umwagiliaji mzuri unahitajika ili kupata vitunguu bora. Umwagiliaji
wa maji
yanayokwenda chini kiasi cha sentimeta moja au zaidi kwa
wiki ni mzuri kwa
kupata vitunguu vikubwa. Epuka umwagiliaji
kupita kiasi au
pungufu kwani hali hii huweza kusababisha
mipasuko.
Udhibiti wa
magugu
Ukuaji na mavuno
yanaathirika sana endapo magugu hayata dhibitiwa
mapema. Magugu
yanadhibitiwa kwa kutumia madawa ama jembe
dogo la mkono.
Wakati mwingine ni mchanganyiko wa madawa,
jembe la mkono na
kungolea kwa mkono.
Udhibiti wa
magonjwa
1. Ugonjwa wa
doa la pinki (Purple blotch)
linaongezeka ukubwa na kufanya rangi ya pinki. Kiini cha
ugonjwa huu huanzia kwenye mbegu na pia hubaki kwenye maozo ya
majani ya vitunguu. Aina ya Red Creole inaonyesha kutoshambuliwa
sana na ugonjwa huu.
Mbinu za kudhibiti ugonjwa huu ni kuendesha mzunguko (croprotation) wa muda mrefu wa mazao pamoja na kuzuia kutuama
kwa maji shambani. Kupunguza msongamano wa mazao shambani na matumizi ya mbolea zenye calcium, phosphate and potassium
hupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. Kwa upande mwingine, matumizi ya mbolea ya nitrojeni kwa wingi au kwa kiasi
pungufu uongeza mlipuko wa magonjwa. Viatilifu kama vile Mancozeb hutumika kuzuia mashmbulizi ya ugonjwa huu.
2. Ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downymildew)
Magonjwa haya hushambulia majani ya mimea shamabani na hata miche michanga. Kwenye majani kunaonekana vidoa vyeupe hasa kwenye majani makuu ya mimea michanga. Ukungu mweupe unatokea na kuongezeka kwa haraka kwenye sehemu au nyakati
za baridi. Viini huishi kwenye mabaki ya mimea ya vitunguu na
huweza kupeperushwa mbali na upepo. Kwenye mimea michanga ugonjwa unaweza kudhibitiwa na madawa kama mancozeb.
3. Kuoza kwa vitunguu (bulb rots)
Ugonjwa huu ni hatari zaidi kwenye sehemu za joto na zenye
kutuamisha maji. Ni vyema kuhakikisha kwamba shambani hakuna
hali ya kutuamisha maji na pia kwenye ghala kunakuwa na hali
nzuri
ya mzuunguko wa hewa.
Udhibiti wa wadudu
Utitiri wa vitunguu (Onion thrips), Funza wa vitunguu(Onionmaggots)
na Minyoo wa vitunguu (Onion wireworms) ni miongoni
mwa wadudu wasumbufu kwenye zao la kitunguu.
1. Utitiri wa vitunguu (Onion thrips)
Hawa ni wadudu wadogodogo sana ambao hula kwa
kukwaruza juu ya jani na kunyonya majimaji ya kwenye mmea. Hali husababisha kutoka kwa mikwaruzo meupe kwenye majani ya vitunguu. Mashambulizi yakizidi majani huanguka
na kunyauka. Ukubwa wa
vitunguu hupungua. Hili ni tatizo kubwa zaidi hasa
wakati wa ukame kuliko wakati wa unyevu.
2. Bungua weupe (White grub)
Huyu ni aina ya
funza mkubwa. Hutaga mayai yake kwenye uozo wa majani na samadi na hivyo mashamba ya vitunguu yaliyoko
karibu au kwenye maeneo ya jinsi hiyo huwa kwenye hatari zaidi.
Hushambulia mizizi na kusababisha kukauka kwa mimea.
Kutifulia
shamba na kuwaweka wazi wadudu hawa kunapunguza idadi yao.
3. Minyoo ya vitunguu (Onion wireworms)
Hawa ni funza ambao mayai yao hutagwa kwenye maeneo yenye
magugu. Wadudu hawa huwa ni tatizo kubwa kwenye sehemu zenye
kutuamisha maji. Kutifulia udongo ili upitishe maji vizuri
pamoja na
udhibiti wa maguu ni njia nzuri ya kuwadhibiti wadudu hawa.
Uvunaji
Inapowezekana mwezi mmoja kabla ya kuvuna udongo uanze
kuondolewa polepole ili kuviacha wazi vitunguu kwa ajili ya
ukaukaji mzuri. Zoezi hili linalenga kufanya angalau
theluthi moja ya
sehemu ya kitunguu kiwe hakijafunikwa na udongo kwa siku
kati ya
7 hadi kumi kabla ya kuvuna ili kuharikisha ukaukaji. Vuna
wakati
asilimia 75 ya shingo za vitunguu zimelala. Mara nyingi
vitunguu
hung’olewa na kurundikwa kwenye matuta na baadaye kukusanywa
na kuwekwa kwa ajili ya kukata shingo. Mizizi pia
inapunguzwa na
vitunguu vinajazwa kwenye magunia tayari kwa kusafirishwa
nyumbani kwa ukaushaji zaidi na kisha kuwekwa galani au
kuuzwa.
Ukaushaji
Madhumuni ya kukausha ni kuvifanya vitunguu visiweze kuota
kwa
muda na pia kuvifanya visiharibike. Vitunguu vilivyokauka
vizuri
huwa na shingo iliyonywea vizuri na ganda kavu. Kama shingo
ya
kitunguu haikukauka sawasawa kutatokea hali ya uozo.
Soko la vitunguu
Ukubwa wa vitunguu ni sifa ingaliwayo na wanunuzi. Vitunguu
vidogodogo sana au vinene sana huwa havipendwi. Vitunguu
vinavyopendwa ni vile vyenye wastani wa unene wa sentimita
nne.
Vitunguu vilivyochubuka, mapacha na vyenye shingo ya chupa
huwa
havipendwi. Vitunguu vilivyooza na vile vilivyobabuka na jua
pia
havifai. Kwa Tanzania wakulima wengi wanauza vitunguu kwa
vipimo vya magunia na ama ndoo za plastiki. Kwa miaka kadhaa
vitunguu vimekuwa vikiuzwa kati ya shilingi 20,000/= hadi
30,000/=
kwa gunia.
Hifadhi ya vitunguu
Vitunguu vipya vilivyovunwa huwa havioti upesi. Hifadhi
sahihi
hurefusha muda wa kutoota. Kwenye hifadhi ni vizuri vitunguu
vipate hewa yenye mzunguuko mzuri na ndiyo maana maghala ya
kuhifadhia vitunguu yanajengwa kama vichanja ili kuruhusu
hewa
kuzunguuka hata kwa kupitia sehemu za chini. Ndani ya ghala
vitunguu humwagwa na kusambazwa kama inavyonyesha kwenye
picha namba.. Vitunguu vinaweza kuhifadhiwa kwa miezi sita
au
zaidi bila kuharibika.
Mavuno
Mavuno ya vitunguu yanategeme huduma za shamba pamoja na
hali
ya hewa. Vitunguu pia hutofautiana katika mavuno kulingana
na aina
ya kitunguu. Kwa wastani vitunguu vinaweza kutoa mavuno kati
ya
magunia 70 mpaka 90 kwa hekari moja.
No comments:
Post a Comment