Tuesday, November 27, 2012

Helemu / korestelori (CHOLESTERAL).


Kipimo cha helemu cha watu waliokuwa na afya nzuri (katika jaribio) kilishuka kwa wastani wa asilimia 10 katika muda pungufu ya masaa mawili baada ya kunywa bilauri moja (ounce 16) yenye vijiko viwili vikubwa vya mdalasini iliyochanganywa na chai ya moto. Kwa kunywa Kinywaji hiki kutwa mara tatu hufanya kazi nzuri ya kushusha kiwango cha helemu mwilini
Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta yanaweza kudhbitiwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai hii pamoja na chakula chako. Hii imeripotiwa na mtafiti maarufu Dr Alexander Andreyed na Eric Vogelmann. Ugunduzi wao uliyakinishwa kwenye jarida mashuhuri la kitiba la Denmark July 1994. Vilevile / aidha uchunguzi mwingine ulibayanishwa kutoa matumizi ya kila siku ya asali Safi hupunguza viwango vya helemu 
 Asali Hupunguza Helemu / Kolesteroli

Kumekuwa na taarifa na ripoti nyingi kuwa Asali hupunguza kiwango cha Helemu. Hebu tijiulize kwanza Helemu / kolesteroli ninini?  Helemu ni aina ya mafuta yanayozalishwa kwenye Ini na hutumika katika uzalishwaji wa Vitamini D na baadhi ya Homoni, kutengeneza ukuta wa CELL na pia utumika ktk utengenezwaji wa chumvi chumvi ya Ngongo ambayo hii husaidia umeng’enywaji wa mafuat (fat.) Ini lina uwezo wa kuzalisha aina hii ya Mafuta yaani Helemu ya kutasha kila siku na inakadiliwa kutowa kiasi cha (milligram 1,000 kwa siku). Hivyo hakuna sababu za kutia mashaka kwamba kunauhitaji wa kutumia virutubisho kuongeza Helemu. Kimsingi aina nyingi ya vyakula zinamchanganyiko wa Helemu na wakati mwingine ni vigumu kujua kama miili yetu hupokea zaidi ya kiwango kinachotakiwa mwilini ambacho kitapelekea Hali mbaya kiafya. Mayai, Nyama, na vyakula vyote vya maziwa kama (cheese na Ice cream) vina wingi wa Helemu wakati vyakula vya mbogamboga, matunda na mbegu havina. Helemu haiwezi kusafirishwa ndani ya Damu mpaka pale ambapo inapo ungana na aina ya protein, ambapo huungana ili kuwezesha usafiruishwaji sehemu mbalimbali za mwili. Wakati Helemu na Protein zinapoungana hutengeneza muunganiko uitwao LIPOPROTEIN. Helemu nyingi sana ni Mbaya na hizi hujulikana kama LDL ( Low Density Lipoproteins) Helemu hii huganda ndani ya kuta za mishipa ya Damu na kuifanya kuwa miembamba, hii ni ile mishipa aina ya Arteries  inayopeleka damu kwenye Moyo, Ubongo, Figo na Utumbo. Na kwa sababu hii ni muhimu sasa kuanza kuwa makini na kiwango cha Helemu kwa kuweka sawia Uzito wa mwili, kufanya mazoezi, kwa afya ya Moyo na kupunguza ama kuepuka kula vyakula vyenye wingi wa mafuta hasa ya wanyama na kuanza kutumia vyakula vyenye Mafuta kidogo na Helemu kidogo mfano Matunda, mikinde, mbegumbegu na samaki. Ukila Kwa wingi vyakula vya wanga pia utakuwa umepunguza ulaji wa vyakula vyenye Helemu nyingi. 
 
Mchanganyiko wa chakula cha Asali na Helemu huru umejumuishwa katika world of healthy foods. Siyo hivyo tu kwamba Asali Haina Helemu bali pia, imeripotiwa kuwa kuweka kiasi kidogo cha Asali katika mlo husaidia kufanya Helemu kuwa katika kiwango sawia. Madini Kama Potassium, Calcium, Sodium na Vitamin B Complex pia huwa katika kiwango sawia, Asali hufahamika kama mpambanaji wa Helemu- Asali hupunguza uwingi wa Helemu kwenye Damu. Antioxidants ndani ya Asali huzuia Helemu iliyo kwenye mzunguko wa Damu kuganda katika kuta za mishipa ya Damu. Matumizi ya kila siku ya Asali hutusaidia kuongeza kiwango cha Antioxidants za ulinzi katika mwili.  

Inaaminika ya kwamba Asali ina uwingi wa Antioxidants kiwango sawa na mbogamboga za kijani kama vile broccoli na spinach ukilinganisha na Matunda kama Apples, Ndizi, Mchungwa na Strawberries. Kwa Ujumla Inasemekana kuwa Asali Nyeusi inauwezo mkubwa zaidi wa kupunguza Helemu zaidi ya Asali nyeupe. Mfano Buckwheat honey ina kiwango kikubwa cha Antioxidants. Matumizi ya Asali na Mdalasini wa pamoja hutowa matokeo mazuri katika kusaidia watu wenye tatizo la kisukari na Wenye kiwango kikubwa cha Helemu.
Hivyo basi jaribu kuona kama Asali inauwezo wa kupunguza Helemu, tumia mchanganyiko wa Asali na Limao, (honey and lemon) : changanya vijiko viwili vidogo vya Asali na nusu limao ndani ya nusu kikombe cha maji ya moto na unywe kila siku asubuhi kabla ya chai / kifungua kinywa. Pia jumuisha Asali katika kila mlo wako mfano badala ya kuweka sukari kwenye chai tumia Asali tumia asali na ndani ya muda mfupi utaona mabadilko na kuongezeka kwa Antioxidants compounds nadani ya mwili wako.

No comments:

Post a Comment


widget