Kufunga Jifunze kufunga na umuhimu wake
KUFANYA MAAMUZI (DECISION MAKING)
UFUGAJI
Ufugaji ni njia moja wapo ya kujipatia kipato kwa jamii nyingi za kiafrika, mfano miaka ya karibuni tumekuwa tukishuhudia jamii ya wafanyakazi wanaofanya kazi mijini katika maofisi mbalimbali bado wanajihusisha na ufugaji wa kuku wa nyama/mayai au ng’ombe wa maziwa na hii kwa sehemu huchangia kwa asilimia kubwa kuongeza pato, kama ufugaji utafanyika kwa kuzingatiwa na kwa kufuata kanuni na ushauri wa wataalamu wa mifugo, katika swala zima kuanzia ujenzi, ulishaji, kinga, madawa maalumu, na mazingiza halisia, hii ikijimuisha na hali ya hewa na aina mfugo unaoweza kuhimili mazingira husika
UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI
Ili kuongeza dhamani ya maisha yako ni vyema kila siku jitahidi kufanya kitu kipya ama basi ongeza maarifa Fulani na hii itapunguza vile visivyofaa ambavyo kwa namna moja ama nyingine vimeujaza ufahamu wako. Leo jaribu ufugaji wa kuku wa kienyeji utapata faida na kuongeza value katika maisha yako na jamii yako ni rahisi sana, hebu nikujuze kidogo juu ya kuku wa kienyeji;
Kuku wa kienyeji wanatofautiana kwa umbo na rangi lakini wote wanafanana kwa mambo yafuatayo. Kwanza woteni wadogo kwa umbo na wana wastani wa uzito wa kilo 1 hadi kilo 2 wanapofika umri kamili. Kutaga kwao huwa kwa kipindi, na kwa wastani hutaga mara tatu kwa mwaka. Kuku wa kienyeji hutaga wastani wa mayai 72 kwa mwaka. Kuku wa kienyeji huanza kutaga wakati amefikia kwenye umri wa majuma 20. Kuku hawa wa kienyeji huchelewa kukua na hii huchangiwa na kujitafutia chakula ambacho mara nyingine huwa ni kidogo. Wanafikia uzito wa kilo moja na robo wakati wana umri wa majuma 21. Endapo mfugaji atazingatia ulishaji na utaalamu upo uwezekano mkubwa wakupata mayai mengi zaidi na kuku wenye uzito mpaka kilo 2 na robo.
Pia kuku wa kienyeji wanazo tabia ambazo ni nzuri na zenye faida katika ufugaji.
- Kwanza ni hodari kujitafutia chakula chao wenyewe.(nyongeza huwa kidogo tu yenye muongeeko wa virutubishi muhumu, dawa na kinga)
- Pili wanao uwezo wa kulalia mayai na kuangua vifaranga.(japo unaweza kutumia machine ya kutotoresha vifaranga ili kutoa nafasi kwa kuku kuanza kutengeneza mayai mengine)
- Tatu kuku wa kienyeji wanahimili sana shuruba za magonjwa mengi ya nchi hizi za joto.
- Mara nyingi ni majasiri kwa kujilinda kutokana na wanyama kama vicheche na ndege kama mwewe, ambao huwashambulia mara wanapowaona.
- Kuku hawa hutaga mayai 7-15 kabla ya kuatamia, na endapo atapta lishe bora yenye chokaa au mifupa yakutosha huweza kutaga mayai zaidi. Hivyo kama una kuku 55 na kila mmoja akataga mayai 15 utakuwa na mayai 750 na mayai 275 yatafaa kuwekwa kwenye mashine ( incubator), 475 waweza kula ama kuuza na kila yai la kuku wa kienyeji ni tsh 300 mara 475 ni sawa na 142,500 tsh. Kipato ziada. Kuku hamsini ni kiasi ambacho unaweza kuwa nacho bila ya mashaka yoyote jaribu sasa.
· NB; Zingatia ushauri wa wataalamu na pia endapo unakuku zaidi ya 55 makoo na jogoo 5 mpaka 7 ni vyema ukatafuta machine ya kutotoresha vifaranga yenye uwezo wa kubeba mayai mia na hamsini mpaka mia tatu. Hii itakusaidia kuwa na utajiri mkubwa na thamani ya pekee sana.
For more info juu ya machine bora etc. Tuma barua pepe kwa; mydailyvalues au cellphone +255767109990
KUFUNGA NA UMUHIMU WAKE
Kumbukumbu za kihistoria zinatuambia kuwa kufunga kumekuwa kukifafanywa tangu enzi kwa kusudi la kiafya kwa miaka maelfu iliyopita. Hippocrates, Socrates, and Plato wote walihimiza kufunga kwaajili ya afya mrejeo( health recovery). Bibilia inatuambia kuwa Mussa nabii na Yesu masihi walifunga siku arobaini 40, kwaajili ya kuhuishwa Roho. Pia Mahatma Gandhi alifunga siku 21 ili kuhamasisha heshimana na mapatano baina ya makundi ya dini mbalimbali.
Jifunze zaidi hapa juu ya habari ya Kufunga
Jifunze zaidi hapa juu ya habari ya Kufunga