Friday, July 8, 2011

FOLIC ACID NA UJAUZITO

Folic Acid na Ujauzito


    Kama una mpango wa uzazi kwa siku za usoni unashauriwa kutumia virutubishi vya aina folic acid hata kama unayo Afya ya kutosha na unapata mlo kamili. Na mara baada ya kupata ujauzito endelea kutumia kirutubishi hiki kwa muda wa wiki 12 za ujauzito. Kama utatumia folic acid itapunguza kwa asilimia kubwa athali za kupata mtoto mwenye tundu la uti wa mgongo (spina bifida), midomo iliyopasuka(cleft lip and palate) na kujifungua kabla ya siku kutimia (premature labour).
Folic acid ni nini?
Folic acid (folate) ni vitamin na inatumika kwaajili ya kutengeneza chembe hai mwilini.             Mwili hauhifadhi folic acid kwa wingi, hivyo unahitaji kila mara ili kukufanya mwenye afya vivyo hivyo wanawake kwaajili ya mtoto tumboni. Kipindi cha mwanzoni cha ukuwaji wa mtoto tumboni ni muhimu unahitaji folic Acid.

Vipo vyakula vingi ambavyo vina mchanganyiko wa folic Acid mfano spinach, sprouts, broccoli, maharagwe (green beans), na viazi (potatoes) canned corn, enriched pastas and breads, juice ya machungwa (orange juice), na avocados. oatmeal, asparagus, romaine lettuce, na lima beans.
Zipo faida nyingine unapotumia folic Acid
·         Mgawanyiko sawia wa chembe hai mwilini na utendajikazi (Proper cellular division    and function)
·         Utengenezwaji wa wekundu wa damu ulio sawia (Proper formation of haemoglobin)
·         Kupunguza athali za shinikizo la damu na magonjwa ya moyo (Reduced risk of heart attack and stroke)
·         Ulizi kwa baadhi ya aina ya kansa; mfano kansa ya shingo ya uzazi na kansa  ya njia ya haja kubwaProtection (colon and cervical cancer)
·         Inapunguza athali za ugonjwa wa Alzheimer’s  
Virutubishi Folic acid kabla na wakati wa Ujauzito
Kama vidonge vya folilc Acid (virutubishi) vitatumiwa katika siku za mwanzoni za ujauzito unapunguza athali ya mtoto kuzaliwa na tatizo la uti wa mgongo kama vile tundu( spina bifida). Hii ni kwa sababu maendeleo ya uti wa mgongo wa mtoto ya awali awapo tumboni yanahitaji folic Acid yakutosha. Pia upo ushahidi unaoonyesha kuwa folic Acid inapunguza athali za kupata mtoto mwenye midomo iliyopasuka, magonjwa ya moyo(congenital heart disease) na kujifungua kabla ya siku(preterm or early)labour.

kimsingi inashauriwa kuanza matumizi ya folilc Acid pale tu unapofikili kuwa wataka kuwa mjamzito katika siku za usoni na kama ujauzito haukupangwa imetokea tu basi anza mara
ujigunduapo umeshika mimba na uendelee kutumia kwa kipindi cha wiki kumi na mbili za ujauzito (12 weeks).
Ni (dozi) kiasi gani kwa siku?
  • Kwa wanawake wengi ni 400 micrograms (0.4 mg) kwa siku.
  • Kama una moja wapo za dalili za hatari zifuatazo ni vyema kutumia dozi ya juu kidogo 5 mg kwa siku
    • Kama uliwahi pata mtoto mwenye tundu la kwenye uti wa mgongo kwa mimba ya hapo awali.
    • Mume ana tatizo kwenye uti wa mgongo
    • Unatumia dawa za kifafa
    • Una kisukuri, sickle cell anaemia, au thalassaemia
Unaweza pata wapi kirutubishi cha folic Acid?
Tembe za folic Acid zinapatikana kwenye maduka ya dawa yote na pia hutolewa bure katika kliniki za huduma ya mama na mtoto RCH/ MCH.
Je kuna madhara yeyote utumiapo folic acid?
Hapan. Folic acid ni vitamin asilia ambayo mwili unaihitaji na siyo dawa na kwa kuitumia unajihakikishia unapata kiwango cha kutosha kinachohitajika kila siku na hasa unapokuwa mjamzito.  
References
·         Antenatal care, NICE Clinical Guideline (March 2008)
·         Pre-conception - advice and management, Clinical Knowledge Summaries (2007)
·         Folic Acid May Help Prevent Premature Birth - A report on proceedings from Society of Maternal-Fetal Medicine annual meeting 2008
·         Bille C, Murray JC, Olsen SF; Folic acid and birth malformations. BMJ. 2007 Mar 3;334(7591):433-4.
·         Ionescu-Ittu R, Marelli AJ, Mackie AS, et al; Prevalence of severe congenital heart disease after folic acid fortification of grain products: time trend analysis in Quebec, Canada. BMJ. 2009 May 12;338:b1673. doi: 10.1136/bmj.b1673. [abstract]
·         Gardiner HM, Fouron JC; Folic acid fortification and congenital heart disease. BMJ. 2009 May 12;338:b1144. doi: 10.1136/bmj.b1144.
·         Wald NJ, Oakley GP; Should folic acid fortification be mandatory? Yes. BMJ. 2007 Jun 16;334(7606):1252.
·         Hubner RA, Houlston RD, Muir KR; Should folic acid fortification be mandatory?

No comments:

Post a Comment


widget