Wednesday, July 20, 2011

Kufunga / fasting

KUFUNGA NA UMUHIMU WAKE
                Kumbukumbu za kihistoria zinatuambia kuwa kufunga kumekuwa kukifafanywa tangu enzi kwa kusudi la kiafya kwa miaka maelfu iliyopita. Hippocrates, Socrates, and Plato wote walihimiza kufunga kwaajili ya afya mrejeo( health recovery).  Bibilia inatuambia kuwa Mussa nabii na    Yesu masihi walifunga siku arobaini 40, kwaajili ya kuhuishwa Roho.        Pia  Mahatma Gandhi alifunga siku 21 ili kuhamasisha heshimana na mapatano baina ya makundi ya dini mbalimbali.
                  Kufunga ni utaratibu tiba wenye nguvu ambao yaweza kusaidia watu kuponyeka / kupona hali za ugonjwa mkali ama ulio hafifu. Moja kati ya hali zilizozoeleka sana ni kama Shinikizo la Damu BP, Pumu, Allergies, Maumivu ya kichwa ya muda mrefu(chronic headaches), Hali ya mavimbe ya utumbo (ulcerative colitis and Crohn’s disease), irritable bowel syndrome, Kisukari cha ukubwani, Magonjwa ya moyo,                       Magonjwa ya viungo (degenerative arthritis), rheumatoid arthritis, Ngozi (psoriasis, eczema, acne),  uterine fibroids, benign tumours, and systemic lupus erythematosus.
                  Kufunga kunatowa muda wa kutafakari na wakati huo mwili unaendelea na utaratibu wa kujiponya wenyewe na kutia nguvu na kukarabati ogani zilizo athirika ama kuharibika. Taratibu ya ufungaji hutowa fulsa ya mwili kufanya utakasaji wa chembe hai zilizo na msongo wa sumu na mabaki uchafu yasiyo faa.
                  Kufunga husaidia mfumo wa chakula kupata pumziko na muda wa ukarabati na uimalishaji wa mucosal layer, kiwambo chenye afya chafaa sana ili kukiwezesha kuzuia upenyaji wa vimelea vya protein ambavyo havijameng’enywa ilivyo stahili kuingia ktk mfumo wa mzunguko wa damu, na hivyo kufanya ulinzi juu ya madhara ya kikinga(autoimmune conditions), na pia ulinzi zidi ya sumsumu za mfumo wa chakula na kimazingira kuingia kwenye mfumo wa damu.
Mfungo ulio stahili ya hali yako waweza kukufanya hisi kama ifuatavyo;
·  Nguvu zaidi                                                                                                               
·         Ngozi yenye Afya (Healthier skin)                                                               
·         Meno yenye Afya na fizi                                                                               
·         Usingizi wenye viwango vya kiafya (Better quality sleep)           
·         Mfumo safi wa mzunguko wa damu wenye afya stahili                   
·         Kupungua kwa hofu na mashaka                                                                    
·         Kupungua au kwisha kabisa kwa maumivu ya  muscles na viungo(joints)                                    Kupungua au kwisha kabisa kwa maumivu ya kichwa                   
·         Kurekebishika kwa viwango vya Shinikizo la Damu                        
·         Stronger and more efficient digestion                                                          
·         Kurekebishika kwa mfumo wa matumbo                                                  
·         Kupungua uzito wa mwili uliozidi viwango vipasavyo                     
·        Ahuweni kwa hali mbalimbali zinazosababishwa na hali yauzee ama umri kama mifumo ya kinga nafsi (autoimmunedisorders )                                                                                                                                                    
                  Ni vyema  kutambua ya kuwa utowaji sumu na uponyaji unaotokea wakati wa kufunga hufanyika pia wakati mtu akiwa hajafunga.      Ufungaji unaweza kuwa wa msaada kwa watu ambao hawapeni maradhi kwa haraka nawepesi kama wapendavyo, na vivyohivyo ni   muhimu    kutambua   kuwa sehemu ya msingi ni jinsi gani mtu anaishi               baada ya   kufunga maana kufunga kwaweza ufanya mwili wenye afya na nguvu na hali nzuri hivyo msingi ni kuchagua maisha yenye nidhamu katika ulaji.
Maswali ya Msingi ya kujiuliza;
.  Nitajuaje kama nahitaji kufunga?
.  Je nifunge kwa Muda gani?
.  Je ni kila mtu anaweza kufunga?
.  Je kufunga kunaweza ponya aina
     Fulani ya ugonjwa au hali?
.  Je nitaweza kupungua kiasi gani cha uzito?
.  Upo utofauti gani kati ya kati kufunga kwa
   kunywa maji pekee na kufunga kwa kunywa  juice pekee?
.  Hali yangu ya umeng’enyaji wa chakula hauwezi
   kubadilika wakati na  baada ya kufunga na kunisababishia               kuongezeka uzito zaidi?
Kwa msaada na ushauri zaidi (Add value) kutuma ujumbe kwenye barua pepe; david.bleiz@yahoo.com or cell; 0787109990 /0767109990

No comments:

Post a Comment


widget