Sunday, June 19, 2011

SUPU YA CABBAGE

SUPU YA CABBAGE
Kupunguza uzito kwa kutumia supu ya cabbage
   Je! umewahi kufikiri ya kuwa unaweza kupunguza zaidi ya kilo nne za uzito wa   mwili wako kwa siku saba tu kwa kutumia aina ya supu iliyotengenezwa kwa cabbage? Upo uwezekano mkubwa wa kufanya diet hii nani rahisi sana. Taklibani miaka 30 sasa watu ulimwenguni kote wamekuwa wakitumia aina hii ya supu kwaajili ya kupunguza uzito.
Awali ya yote ngoja nikufahamishe faida ya programu hii:
     . Kupungua uzito kwa afya
    .  Kupunguza msongo (stress relief)
    .  Kupunguza adhari za kupatwa na ugonjwa wa kisukari
    .  Kuwa na ngozi yenye muonekano mzuri(youthful skin)
    .  Kinga bora
Supu ya cabbage inaufanya mwili wako kufanya kazi ya ziada wakati wa kumen’genya chakula na hivyo husaidia kutumika kwa mafuta mafuta ya ziada yaliyohifadhiwa mwilini na hivyo kupunguza uzito. 
Jambo la msingi kulifahamu ni kuwa Programu hii hufanyika kwa siku saba tu na zaidi inashauriwa ifanye na watu wazima na siyo watoto au wale walio katika kipindi cha makuzi (adolescents). Mara utakapokuwa umemaliza unaweza kuendelea na programu nyingine za kupunguza uzito taratibu na endapo utahitaji tena kupungua uzito zaidi waweza anza tena supu kwa siku saba. Je uko tayari kuanza sasa?
Mchanganyiko wa maandalizi ya Supu ya Cabbage
     Ingredients: Vitunguu 2, Pilipili hoho 2, Nyanya 2 mbili, Bunch moja la celery
One package of lipton Onion Soup Mix, Cabbage moja
Katakata vitu vyote hivi kisha weka katika chungu chenye maji ya moto pika kwa dakika kumi mpaka ishirini pia waweza ongeza radha ya supu kwakuweka chumvi kiasi, garlic ya unga na spice uzipendazo .
Diet hii inapaswa kufuatwa kwa mpangilio ili kupata matokeo mazuri
Siku ya Kwanza 1
Kula matunda ya aina yote unayoyataka, isipokuwa ndizi. Kwa siku ya kwanza na pia waweza kunywa juice na maji ya kutosha.
Siku ya pili 2
Waweza kula aina zote za mbogamboga aina ya kijani ila epuka kula maharagwe, paes, matunda hayaruhusiwi siku ya pili
Siku ya tatu 3
Tumia aina zote za supu, matunda na mbogamboga.
Siku ya nne 4
Waweza kula ndizi nyingi uwezavyo zaidi ya nane na kunywa maziwa yakutosha wakati ukiendelea kutumia supu ya cabbage, na hii ni kwaajili ya kupunguza hamu ya vitu vitamu.
Siku ya tano 5
Kula ounces 10-20 ounces za nyama na pia waweza kula nyanya sita za ukweli. Kunywa maji aghalabu bilauli 6 mpaka 8 ili kusaidia kusafisha na kuondoa uric acid ndani ya mwili.
Siku ya sita 6
Kula nyama na mbogamboga pamoja na supu ya cabbage
Siku ya saba 7
Kula brown rice, mbogamboga na juice ya matunda isiyo na sukari pamoja supu ya cabbage.

No comments:

Post a Comment


widget