Kukatika kwa nywele
Asali
ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa
kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork.
Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika
15.
Mzunguko wa Ukuwaji na Nywele
Mzunguko
wa kawaida wa ukuwaji wa
nywele hufikia ukomo kati ya miaka miwili mpaka sita na kila nywele hukuwa kwa
makadilio ya sentimeta moja kila mwezi. Inakadiliwa kuwa kila mtu hupoteza
kiasi cha nywele 20 mpaka 100 kila siku; ingawaje kwa baadhi ya watu hupatwa na
hali ya kupoteza nywele nyingi zaidi ya kawaida. Kwa Wanaume au Wanawake
upotevu wa nywele si jambo la kufurahisha hata kidogo. Nywele kama Taji la
Utukufu wakati wote limempatia mtu uwezo wa kueleza hisia zake kwa njia za
mitindo mbalimbali vile impendezavyo. Upotevu wa nywele waweza kuleta mwitiko
hasi kwa baadhi yetu na ukosefu wa kujiamini na hata kuleta hisia za muonekano
wa umri mkubwa wakati bado wakati.
Zifuatazo ni baadhi ya sababisho ya Upotevu wa Nywele Isivyokawaida.
a) ALOPECIA inaaminika kuwa ni moja ya sababu ya awali na
msingi inayoleta upotevu wa nywele mapema kwa wanaume na wanawake. Nywele huwa
nyembamba na kusinyaa kisha kukatika, zipo aina mbalimbali za Alopecia.
b) Upungufu ama hali ya
kutokuwepo Uwiano sawia wa vichocheo (Homoni) za kiume ama za kike mwilini
zijulikanazo kama; ANDROGENS na ESTROGENS.
Mfano wapo wanawake ambao
hupoteza nywele nyingi san wakati wa Ujauzito ama mara baada ya kujifungua.
Wakati wa ujauzito Uwepo wa kiwango cha juu wa moja wa Homoni waweza kuleta
nywele kakatika kwa hali ya kawaida ama isivyokawaida na baada ya kujifungua nywele huweza kutatika isivyo kawaida kisha
Huanza kuota kawaida, katika Hali kama hii hakuna haja ya kutumia Dawa kwa
ajili ya kuotesha nywele.
c) Dawa (Medication)
baadhi ya madawa yenye kiwango kikubwa cha vitamin A mfano vidonge vya
virutubisho, dawa za matibabu ya shinikizo la Damu, Gout, Vidonge vya majira,
na Dawa za Msongo wa Akili. Pia matibabu ya kansa na ndiyo maana wagonjwa wengi
wa walio katika Matibabu ya Kansa hushindwa kukaa na nywele na kucha wakati wa
matibabu.
d) Upotevu wa nywele unatokana
kama sehemu ya Dalili ya hali ya kiafya kama Upungufu wa wa Wekundu wa chembe
nyekundu za Damu ( Anaemia), Lupus, au KISUKARI ( Diabetes) . Kwa kuwa Upotevu
wa nywele waweza kuwa ni Dalili ya awali ya Ugonjwa, hivyo ni muhimu kutafuta
sababisho mapema na kutibiwa wa wakati. Kwenye matatizo kama ya Thyroid Gland
nywele zaweza kukatika sana.
e) Hali ya Msongo yaweza kuleta hali ya upotevu wa nywele ijapokuwa
si kawaida sana hii kutokea
f) Hali ya magonjwa kama Mapunye. Au psoriasis ya kichwani huweza kleta upotevu wa
nywele.
Kukatika kwa nywele Matibabu jinsi ya kuandaa mchanganyiko
a. Tengeneza
mchanganyiko wa mafuta ya mizeituni (Olive Oil) kiasi katika
hali ya uvuguvugu, changanya pamoja mdalasini na Asali kijiko kidogo kimoja
kimoja kisha paka kichwani na massage eneo hilo na acha kwa dakika 15-20. Osha
na maji Rudia kufanya hivi mara tatu mpaka nne kwa wiki.
b. Changanya kijiko kidogo kimoja cha Asali na glasi
ndogo ya brandy au vodka pamoja na Juice ya kitunguu maji na upake kichani
usiku kucha funika na kitambaa au kofia, kesho yake osha na Sabuni vizuri.
c. Pia changanya robo kikombe cha juice ya kitunguu
maji na Asali mbichi kisha paka kichwani kwa mtindo wa uchuaji (massage) fanya
hivi kila siku usiku.
d. Fanya
uchauji kichwani (Massage) kwa kutumia mchanganyiko wa Asali na kiini cha yai
kisha acha kwa muda wa nusu saa kisha osha na maji na sabuni.
No comments:
Post a Comment