Tuesday, August 2, 2011

sonona

Sonona (Depression)                               





    Sonona ni hali inayompata mtu kimfumo usio na mpangilio kiufahamu inayoambatana na kujihisi huzuni, hii inayoweza kuchukuwa wiki mbili au zaidi, hali yakupoteza hamu ya kuishi, upweke, kukosa tumaini. Hali hizi zinaweza kumuathili mtu katika utendaji wa kazi za kila siku.
Sonona inaathiri ufahamu , lakini hiyo haimaanishi kichwa chote,” Sonona ni ugonjwa wa kimedical unaohusisha mabadiliko ya mfumo wa biokemikali(biochemistry) wa ubongo.
Sonona siyo udhaifu wa kitabia, na wala haina maana kuwa muathilika hana uwezo wa kufanya kitu chochote. Ila Sonona ni hali au ugonjwa wa  kimedikali( medical illnes) kama magonjwa mengine mfano kisukali au vidonda vya tumbo, na hivyo siyo kitu chakudhalau ni muhimu kwa mgonjwa kupata matibabu stahili  na kwa wakati. Sonona inatibika kikamilifu maana karibu asilimia tisini 90% ya watu wanaopatwa na hali hii hutibiwa kabisa kwa njia ya vidonge na counselling au psychotherapy na kupona
Aina za Sonona; kuna ujumla wa aina nne za sonona nazo ni kama ifuatavyo;
  • Sonona Kuu(Major depression), pia inajulikana kama melancholia, hali hii mtu aweza kudumu nayo hata kwa mwaka mzima kama haikutibiwa, mtu mwenye hali hii hupata uchovu, maumivu ya kichwa, na maumivu mengine na kukosa hamu ya kula na vyote hivi huja kwa vipindi.
  • Bipolar disorder, pia inajulikana kama manic, husababisha kubadilika badilika kwa tabia isivyo kawaida. Mtu mwenye aina hii iliyo kithili anaweza kuona vitu ama kusikia sauti, ambavyo kihalisia haviko kabisa mahali alipo hivyohivyo wakati  mwingine kuhisi hatari isivyo kweli (paranoia).
  • Dysthymia hii ni hali ya muda mrefu na mara nyingi humuanza mtu tangu akiwa mtoto mdogo ama wakati wa makuzi(adolescence) na inaweza kudumu kwa muda mrefu sana kama haitatibiwa kwa wakati.
  • Sonona msimu(Seasonal) huwapata hasa watu walioko maeneo ya uwanda wa hemisphia ya kaskazini wakati wa upungufu wa jua pale panapokuwa na muda mfupi wa jua.
Dalili za Sonona(Depression) ni zipi?
  • Huzuni inayoendelea(Persistent sadness).
  • Kusikia hali ya kuwa na hatia, kujiona haustahili(huna thamani) huna msaada na haufai kitu.
  • Kupoteza hamu/ hari ya vitu unavyovipenda na kukosa furaha ya mambo kama ngono
  • Kupoteza au kuwa na kumbukumbu hafifu na kushindwa kuwa na umakini kifikira.
  • Hali ya ugonjwa uliopo kuwa mbaya zaidi mfano kisukali au arthritis.
  • Kulala muda mrefu (oversleeping or Insomnia)
  • Kuongezeka uzito au kupungua.
  • Uchovu na kukosa nguvu
  • Wasiwasi, Shaka, kujitikisa tikisa, hasira za haraka
  • Kuwa na mawazo ya kujiua
  • Kuongea taratibu hali kadharika kutembea.
  • Maumivu ya kichwa, tumbo, pia shida katika mfumo wa chakula.

Sonona kwa wanaume (Depression in Men)
Kimsingi hapo awali sonona ilitambulika kama ugonjwa wa “wanawke’’ lakini ukweli ni kwamba hali hii ina athili jinsia zote mbili, na inapompata mtu inaleta muingiliano wa kimahusiano ya mtu katika kazi na shughili zake za kila siku. Dalili za sonona kwa wanawake na wanaume ni sawa ila wakati mwingine wanaume wanaweza kuwa wakali na wepesi kukasirika
Kwanini si rahisi kugundua Sonona kwa wanaume?
Zipo sababu mbalimbali za kwanini dalili za sonona hazijidhihirishi kirahisi kwa wanaume, mfano; wengi wa wanaume huwa na tabia ya kukataa kuwa wanatatizo kwasababu wnapaswa kuwa mashupavu(strong) na majasiri, hii ni matokeo ya kimila na jadi kuwa wanaume wapaswa kuwa wakakamavu. Kwa hivyo wengi hupenda kusema wanajisikia uchovu. 

Je Sonona inaathili hali ya ngono(jimai) na utendaji tendo?     Ni kweli kwa wanume sonona huathili hamu ya kufanya ngono na utendaji tendo zima kwa sehemu kubwa sasna. Hali kadharika hata dawa zinazotumika kutibu sonona pia, ijapokuwa si rahisi wanamume kuzungumzia hali ya upungufu hasa juu ya ufanyaji tendo, wengi hudhani ni hali yao ya kimaumbile udhani huu si sahihi.
Madhara ya sonona kwa wanaume isipotibiwa.  Ripoti nyingi zionyesha wengi wa wanaume wenye sonona hujiiwa na hufanikiwa kirahisi kuliko wanawake, unywaji pombe ulio kithiri na utumiaji wa madawa ya kurevya, ndoa kuvunjika na muongezeko wa matendo ya jinai.       
 Matibabu
Sonona inaweza kutibiwa kwa njia  ya Dawa au Ushauri ama vyote viwili kwa pamoja,
Kwa Sonona ya chini naya ya kati Ushauri (counselling) waweza kuwa matibabu mazuri zaidi. Kwa sonona kuu matibabu jumuisho ya dawa na ushauri yafaa zaidi kwa muendelezo wa miaka miwili, hii hupunguza kutokurudiwa tena na sonona.
Kama Una sumbuliwa na Sonona si rahisi kujua ni kwanini imekupata na kwa kesi nyingi za wagonjwa zinazojitokeza husababishwa na sababu zaidi ya moja ambapo yaweza ikawa ni genes, matukio ya zamani, na hali maisha ya sasa na athali nyingine.
Hivi ni baadhi ya vitu vinavyoweza kuchangia hali ya Sonona sababisho chochezi(causes)
  • Kibailojia (Biology). Bado kufahamika hasa ni kitu gani hutokea kwenye ubongo wa mtu aliyepatwa na sonona. Ila baadhi ya stadi zinaonyesha kuwa sehemu Fulani ya ubongo kutokufanya kazi ipasavyo na pia inaweza kuathiliwa na mabadiliko ya kiwango cha kemikali fulani katika ubongo ziitwazo neurotransmitters.
  • Genetics. Watafiti wanaonyesha kuwa kama Sonona imeathili moja ya wanafamilia ni rahisi kufuata wengine ama urahisi wakupata unakuwa ni mkubwa kwa wengine wa familia hiyo.
  • Jinsia. Stadi zinaonyesha kuwa wanawake huathiliwa na sonona mara mbili zaidi ya wanaume, hakuna anayefahamu ni kwanini hasa hili hutokea, ila mabadiliko ya homoni katika mwili wa mwanamke kwa wakati tofauti huenda ikachangia.
  • Umri. Watu wenye umri mkubwa wako kwenye athali kubwa ya kupata Sonona. Hii ni kwa husababishwa na sababu nyingi mfano kuishi pweke/pekee, kukosa msaada wa kijamii nk.  
  • Hali za kiafya. Magojwa kama kansa, magonjwa ya moyo, goita,maumivu ya mwili ya muda mrefu na mengineyo mengi.
  • Kuumizwa na huzuni( grief). Mfano unyanyasaji wa kijinsia na kimwili pia vilivyotokea mwanzoni wakati wa utoto ama karibuni. Pia huzuni baada ya kufiwa na rafiki au mpenzi ama ndugu.
  • Msongo na hali ya mabadiliko. Siyo jambo la kushangaza mtu kupata sonona anapokuwa na msongo mfano wakati wa talaka( matengano) ama wakati wa kuuguza mgonjwa, na pia hata hali cahnya kama kuoa, kupata kazi mpya pia yaweza sababisha sonona. 
  • Matibabu. Aina nyingi za dawa husababisha dalili za Sonona.Many prescription drugs can cause symptoms of depression. Pombe na matumizi ya vitu vya hatari ni kawaida sana kwa  mtu mwenye sonona na hivi hufanya hali kuwa mbaya zaidi!
Unahitaji kutumia dawa kwa muda gani?
Unahitaji kutumia dawa kwa muda kutegemeana na hali yako ya sonona na pia daktari wako anaweza kukupatia dawa kwa uchache wa miezi sita mpaka tisa ama zaidi, inafaa kutumia dawa kwa muda mrefu ili kupunguza uwezekano wakujirudia tena ni vyema kuzungumza na tabibu wako juu ya dawa au swali ulilonalo?
Mambo yakufanya ili kuepuka/kundokana na Sonona.
  • Jitegemee. Usitegemee kufanya kila kitu kile ambacho unaweza kufanya. Weka ratiba / taratibu za utendaji wako.
  • Usiamini mawazo potofu ambayo wawezakuwa nayo, kama kujilaumu mwenyewe, au kutegmea kushindwa kwa jambo ulilopanga hata kabla ya kulifanya
  • Jihusishe na shughuli zinazokufanya kujisikia vyema na kukufanya kujiona umefanikiwa.
  • Epuka kufanya maamuzi ya maisha ya juu uwapo na sonona, na kama inakupasa kufanya hivyo shauriana na mtu unayemuamini kwa msaada zaidi.
  • Jiepushe na madawa na pombe. Maana husababisha hali kuwa mbaya zaidi
  • Mazoezi ya viungo yameonyesha huleta mafanikio kuondoa hali mbaya ya msongo, fanya mazoezi mara 4 mpaka 6 kwa wiki, kwa uchache wa dakika 30 lkn hata zoezi kidogo lafaa sana.                                           
  • Usikubali kukata tamaa kirahisi.
 
 Kwanini mtu mwenye sonona apate msaada mapema.
  • Mtibabu ya mapema hupunguza athali za mgonjwa wa Sonona kuwa mbaya.
  • Hisia za kujiuwa huwa za kubwa sana kwa watu wenye sonona hivyo wanapopatiwa matibabu mapema ni rahisi kuondikana na hisia hizo.
  • Matibabu yanaweza kumsaidia mgonjwa kurudi katika hali yake ya kawaida  na kuendelea kufurahia maisha.
  • Matibabu husaidia kukinga sonona kujirudia tena.


Jifunze juu ya Mning'inio                                               Ukurasa Uliopita

No comments:

Post a Comment


widget