Kipimo cha
helemu cha watu waliokuwa na afya nzuri (katika jaribio) kilishuka kwa wastani
wa asilimia 10 katika muda pungufu ya masaa mawili baada ya kunywa bilauri moja
(ounce 16) yenye vijiko viwili vikubwa vya mdalasini iliyochanganywa na chai ya
moto. Kwa kunywa Kinywaji hiki kutwa mara tatu hufanya kazi nzuri ya kushusha
kiwango cha helemu mwilini
Madhara
yaletwayo na vyakula vyenye mafuta yanaweza kudhbitiwa kwa matumizi ya mara kwa
mara ya chai hii pamoja na chakula chako. Hii imeripotiwa na mtafiti maarufu Dr
Alexander Andreyed na Eric Vogelmann. Ugunduzi wao uliyakinishwa kwenye jarida
mashuhuri la kitiba la Denmark July 1994. Vilevile / aidha uchunguzi mwingine
ulibayanishwa kutoa matumizi ya kila siku ya asali Safi hupunguza viwango vya helemu
Asali Hupunguza Helemu / Kolesteroli
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEitmfDX800QuqHzX0f1iYhHaS42oKLL1O1DDPPvM3TPHn3oYmSLpGXCJOu3lAJuwdaeEBgqrNZyFOHwjT4YCqZ0N7piBQs8lY8u3D-ATgbw8AjW4PEx_7YZgpsVB3Q_uUCsT-O4duFHddLf/s1600/mdalasini+joint+pic+6.png)
Mchanganyiko wa chakula cha Asali na Helemu huru
umejumuishwa katika world of healthy
foods. Siyo hivyo tu kwamba Asali
Haina Helemu bali pia, imeripotiwa kuwa kuweka kiasi kidogo cha Asali katika
mlo husaidia kufanya Helemu kuwa katika kiwango sawia. Madini Kama Potassium,
Calcium, Sodium na Vitamin B Complex pia huwa katika kiwango sawia, Asali
hufahamika kama mpambanaji wa Helemu- Asali hupunguza uwingi wa Helemu kwenye
Damu. Antioxidants ndani ya Asali huzuia Helemu iliyo kwenye mzunguko wa Damu
kuganda katika kuta za mishipa ya Damu. Matumizi ya kila siku ya Asali
hutusaidia kuongeza kiwango cha Antioxidants za ulinzi katika mwili.
Inaaminika ya kwamba Asali ina uwingi wa Antioxidants kiwango sawa
na mbogamboga za kijani kama vile broccoli na spinach ukilinganisha na Matunda
kama Apples, Ndizi, Mchungwa na Strawberries. Kwa Ujumla Inasemekana kuwa Asali
Nyeusi inauwezo mkubwa zaidi wa kupunguza Helemu zaidi ya Asali nyeupe. Mfano Buckwheat honey ina kiwango
kikubwa cha Antioxidants. Matumizi ya Asali na Mdalasini wa pamoja hutowa
matokeo mazuri katika kusaidia watu wenye tatizo la kisukari na Wenye kiwango
kikubwa cha Helemu.
Hivyo basi jaribu kuona kama Asali inauwezo wa
kupunguza Helemu, tumia mchanganyiko wa Asali na Limao, (honey and lemon) : changanya vijiko viwili vidogo vya Asali na nusu limao ndani ya nusu
kikombe cha maji ya moto na unywe kila siku asubuhi kabla ya chai / kifungua
kinywa. Pia jumuisha Asali katika kila mlo wako mfano
badala ya kuweka sukari kwenye chai tumia Asali tumia asali na ndani ya
muda mfupi utaona mabadilko na kuongezeka kwa Antioxidants compounds nadani ya
mwili wako.
No comments:
Post a Comment