Papai hujulikana kwa Lugha nyingine kama Papaya,
Paw Paw, Papaw, Tree Melon (botanical name Carica Papaya), lina umbo kama Yai
la kuku na langi ya kijani manjano, manjano ama rangi ya chungwa lililoiva vizuri.
Papai ni Tunda la mti aina ya mpapai na linaweza kufikia uzito wa kilo mbili na
nusu 2.5kg. Kawaida huwa na Radha ya Uchungu Utamu na lina asili ya Ukanda wa
Tropiko na maeneo yenye Unyevu mfano Mexico, Amerika ya Kati, Afrika, Asia,
Australia nk.
Faida za
kiafya za Papai
Sehemu zinayotumika kama Dawa ni Tunda lenyewe, Mbegu, Shina, maganda na
Majani yake pia. Unapokuwa sokoni, Gengeni ama Dukani unaweza kununua papai katika
hali tofauti tofauti kama majani ya chai, vidonge au Papai lililo bivu, ambalo
linaweza kuliwa kama lilivyo, ama kwa kutengenezwa Juice. Huenda unajiuliza ni
faida gani hizi za Papai? Sawa
tuanze na tunda la papai lina Wingi wa Utomwili, Madini aina ya Folic, Vitamin
A, C na E. Pia papai lina kiasi Fulani cha madini ya Calcium, chuma, Riboflavin,
Thiamine, na Niacine. Pia Papai linauwingi wa Antioxidant nutrients
flavonoids na carotenes, vitamini C, nyingi sana na Vitamin A, na kwa uchache
Calories na Sodium. Uweza kjifunza Aina nyingine ya vyakula vyenye Antioxidant Hapa.
Mti wa Papai Papai/Paw paw ina wingi wa kimeng’enya kwa kimombo-enzymes kijulikanacho
kama papain na chymopapain ambacho husaidia umeng’enyaji wa chakula hasa
aina ya Protein tunayokula kuwa Amino Asidi. Utafiti wa karibuni umeonyesha
kuwa Amino Asidi Huusika na kila kitu kinachofanywa na Mifumo yetu ya mwili kimsingi
mchanyato wa kikemikali mwilini na pia huleta Ujumla wa Afya ya Akili
na Mwili. Jinsi tunavyoongezeka umri na ndivyo mwili Huzalisha
Vimeng’enya kwa Uchache zaidi ndani ya Tumbo na Kongosho, kitendo ambacho
husababisha umeng’enywaji mdogo/ hafifu wa Protein. Na matokeo yake tunapata
wingi wa Protein isiyomeng’enywa kwa wingi ambayo husaidia ukuwaji wa vijidudu
vya maradhi tumboni. Tunaweza kusema kuwa Kiwango chenye ubora cha Protein ni
hasa lazima kwa Afya Zetu na hapo ndipo Kimeng’enya aina ya Papain kipatikanacho
kwenye Papai huwa na Faida kubwa Kwetu na kufanya Umuhimu wa Papai Katika
maisha ya kila siku.
Kimeng’enya cha Papain huzalisha kwenye ganda la Papai, na Hii husaidia Papai
lisiliwe na wadudu wakati wa kuiva, faida nyingine ya papain ni Kupunguza
Uvimbe, Hupunguza Maumivu, hupunguza maumivu ya Magonjwa ya Rheumatoid
arthritis, na Osteoarthitis. Kwa Sababu ya wingi wa Antioxidant ndani ya Papai pia huepusha Cholesterol, pia
hukinga maradhi ya Atherosclerosis, Strokes, Shinikizo la Moyo, kisukari, Saratani na
Magonjwa ya Moyo. Baada ya kumaliza
kutumia Madawa kama Antibiotic kwa Muda ni vyema kula ama kunywa Juisi ya Papai
kila siku ili kurejesha Afya ya mwili na Baadhi ya Bacteria wa tumboni ambao
husaidia ulinzi na umeng’enyaji chakula walio kufa kwa sababu ya matumizi ya
Dawa.
Tafiti
zilizofanywa Kuhusu Papai
Stadi zimeonyesha kuwa Papain husaidia pia kupunguza Athari za matibabu ya
Kansa, zaidi katika kupunguza maumivu wakati wa kumeza isababishwayo vidonda
vya mdomoni baada ya mionzi na dawa, pia hii husaidia kupandisha kinga ya mwili
na kusaidia kupambana na Saratani Zipo Bidhaa ambazo zimetengenezwa kwa Papai mfano bidhaa za kampuni ya
Rochway ya Australian (kwa taarifa zaidi bofya ama vinjari bapa (rochway.com.au) Kwa kujifunza zaidi juu ya Papai /references na juu ya stadi za
karibuni unaweza tazama PubMed Gov. www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/
)
Muhtasari wa Hali zinazoweza kurekebishwa na
Papai
·
-Muongezeko wa kiwango cha Ubora wa Protien
inayohitajika ndani ya Mwili
·
-Huboresha Afya ya mwili na kuufanya kuwa
na nguvu ya kutosha kwa muda mrefu
·
-Huchochea uimarishwaji wa Misuli ya
mwili
·
-Husaidia Mfumo wa mzunguko wa Damu.
·
-Husaidia Uimarishwaji wa Kinga ya
mwili
·
-Husaidia Mfumo wa Umeng’ennyaji wa
Chakula na hasa Protein na Huleta Muongezeko wa Uzalishaji wa Vimeng’enya,
katika usagaji Chakula.
·
-Husaidia tatizo la Kisukari na Asthma.
·
-Mgonjwa wa Kifua Kikuu akila kwa muda mrefu matunda
haya atapona na hutibu kiungulia.
·
-Pia Papai huweza Kutumika kwa nje ya
Ngozi kwaajili ya Vidonda, vipele, kansa ya ngozi na vidonda vya moto, Husaidia
kupona kwa Haraka vile ambavyo vimekuwa sugu. Kwa kutumia utomvu ama maganda
ya papai.
·
-Husaidia Mtu kuzuia kupata Tatizo la mtoto wa Jicho
·
-Kwa sababu uwingi wa Vitamin A, Husaidia watu
wanaovuta sigara kuapatwa na tatizo la Emphysema (kujaa Hewa ndani
ya Mapafu)
·
-Husaidia kupunguza Uvimbe
·
-Husaidia kupunguza Kichefu chefu na Hali ya kupata choo kigumu / kufunga choo
UTARATIBU NA MAANDALIZI YA BAADHI YA SEHEMU
ZITUMIKAZO KUSAIDIA MATIBABU
*Tumia mbegu ambazo ziko fresh 10-12
kuzitafuna kwa siku kwa Muda wa siku Tano hii hutibu Ini.
*Kausha majani ndani ya nyumba palipo
kivuli- haya husaidia kutibu pumu pale inapoanza kubana yachome majani
yaliyokauka kisha jifukize kubana kutaisha.
*Papai lilomenywa na kupondwa vizuri
hufaa kwa uso na hulainisha ngozi likipakwa kama lotion.
*Mbegu zilizokaushwa ndani ya nyumba na kisha
kusangwa na kuwa katika hali ya ungaunga hutibu Malaria
matumizi Tumia kijiko 1 cha chai
changanya na Uji na unywe mara Tatu kutwa kwa siku Tano.
*Mizizi yake ikipondwa na kulowekwa
kwenye maji yaliyochemshwa kiasi cha lita mbili na nusu kwa Dakika 15,
inasaidia kutibu figo, Kibofu cha mkojo na pia husaidia kuzuia kutapika.
Ningependa kupata Taarifa ya wale hasa wamewahi kutumia ama wanatumia kwa
Afya nani sehemu ya mlo wa kila siku ili kuboersha afya zao.
No comments:
Post a Comment