Tuesday, November 27, 2012

Ukosefu wa nguvu za kiume

Asali ina historia ndefu ya kuamsha uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi. Kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji, asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za kimashariki mwa Dunia. Mwaka jana, watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali ina uwezo wa kupeleka mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo kwa mdalasini, katika Africa na dunia ya kusini, mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza stamina zao za kufanya mapenzi.

Wataalamu wana Bainisha:
Tafiti zinaonyesha kuwa! Ukichukua asali vijiko vikubwa vitatu3, mdalasini vijiko vikubwa vitatu 3 na tangawizi vijiko vikubwa vitatu 3 ukichanganya na maji vuguvugu glass 1 kisha ukaiacha kwa muda wa dk 15 hadi 30, kisha ukachuja na kunywa! Huongeza hamu ya kufanya mapenzi, na muda wa mechi huongezeka na uimara katika tendo zima lakini pia mchanganyo huo huongeza joto mwilini na kuongeza raha.
Ugumba:
Asali inaaminika kuamsha nyege na wapenzi wa jinsia zote mbili wanashauriwa kunywa anglao vijiko viwili vya mezani kila siku kabla ya muda wa kulala usiku. Mdalasini umetumika kwa muda mrefu kwenye dawa za kihindi na kichina ili kuongeza uwezo wa uzazi kwakina mama wenye kuhitaji kuzaa. Kiungo hiki (mdalasini) huchanganywa na kiasi cha asali na kufanya mgando (paste) ambao hupakwa kwenye fizi za meno na kunyonywa na kuingia mwilini taratibu. Familia moja iliyokuwa haina watoto iltumia mgando huu kwa mafanikio na kupata mapacha wa kike baada ya kushindwa kwa muda wa miaka 14 kupata mtoto. Walikuwa wameshakata tamaa ya kupata mtoto hadi waliposikia kuhusu mchanganyiko huu wa asali na mdalasini.

No comments:

Post a Comment


widget