KUFUNGA NA UMUHIMU WAKE
Kumbukumbu za kihistoria
zinatuambia kuwa kufunga kumekuwa kukifafanywa tangu enzi kwa kusudi la kiafya
kwa miaka maelfu iliyopita. Hippocrates, Socrates, and Plato wote walihimiza
kufunga kwaajili ya afya mrejeo( health recovery). Bibilia inatuambia
kuwa Mussa nabii na Yesu masihi walifunga siku arobaini 40, kwaajili
ya kuhuishwa Roho. Pia Mahatma Gandhi alifunga siku 21 ili
kuhamasisha heshimana na mapatano baina ya makundi ya dini mbalimbali.
Kufunga ni utaratibu tiba wenye nguvu ambao yaweza kusaidia
watu kuponyeka / kupona hali za ugonjwa mkali ama ulio hafifu. Moja kati ya
hali zilizozoeleka sana ni kama Shinikizo la Damu BP, Pumu, Allergies,
Maumivu ya kichwa ya muda mrefu(chronic headaches), Hali ya
mavimbe ya utumbo (ulcerative colitis and Crohn’s disease), irritable
bowel syndrome, Kisukari cha ukubwani, Magonjwa ya moyo, Magonjwa
ya viungo (degenerative arthritis), rheumatoid arthritis, Ngozi
(psoriasis, eczema, acne), uterine fibroids, benign
tumours, and systemic lupus erythematosus
Kufunga kunatowa muda wa kutafakari na wakati huo mwili
unaendelea na utaratibu wa kujiponya wenyewe na kutia nguvu na kukarabati ogani
zilizo athirika ama kuharibika. Taratibu ya ufungaji hutowa fulsa ya mwili
kufanya utakasaji wa chembe hai zilizo na msongo wa sumu na mabaki uchafu
yasiyo faa.
Kufunga husaidia mfumo wa chakula kupata pumziko na muda wa
ukarabati na uimalishaji wa mucosal layer, kiwambo chenye afya chafaa
sana ili kukiwezesha kuzuia upenyaji wa vimelea vya protein ambavyo
havijameng’enywa ilivyo stahili kuingia ktk mfumo wa mzunguko wa damu, na hivyo
kufanya ulinzi juu ya madhara ya kikinga(autoimmune conditions), na pia
ulinzi zidi ya sumsumu za mfumo wa chakula na kimazingira kuingia kwenye mfumo
wa damu.
Mfungo uliyo stahili yako unaweza
kukufanya kuhisi kama ifuatavyo
·
Utahisi kuwa na nguvu zaidi
·
Ngozi yako itakuwa na Afya nzuri(health skin)
·
Hali ya fizi za meno kuwa na imara na zenye Afya
zaidi
·
Utapata usingizi wenye viwango vya kiafya na si wa
mang’amu ng’amu.(better quality sleep)
·
Mfumo safi wa hewa na mzunguko wa Damu wenye afya
stahili.
·
Kupungua kwa Hofu na mashaka mengi (msongo na
wasiwasi)
·
Kupungua na kuisha kabisa maumivu ya misuli(muscles)
na viungo( joints).
·
Kupungua na kuisha kabisa maumivu ya kichwa.
·
Kurekebishika kwa viwango vya shinikizo la Damu.
·
Mfumo safi wa umeng’enyaji wa chakula unaofanya
kazi kimathubuti( strong and more efficient digestion).
·
Kurekebishika kwa mfumo wa matumbo.
·
Kupungua uzito wa mwili uliozidi viwango vipasavyo
·
Ahuweni kwa hali mbalimbali zinazosababishwa na
hali ya uzee ama umri kama mifumo ya kinga nafsi( autoimmune disorders)
·
Ni vyema kutambua ya kuwa utowaji
sumu na uponyaji unaotokea wakati wa kufunga hufanyika pia wakati mtu akiwa
hajafunga.Ufungaji unaweza kuwa wa msaada kwa watu ambao hawapeni maradhi kwa
haraka nawepesi kama wapendavyo, na vivyohivyo ni
muhimu kutambua kuwa sehemu ya msingi ni jinsi
gani mtu anaishi baada ya kufunga maana kufunga kwaweza
ufanya mwili wenye afya na nguvu na hali nzuri hivyo msingi ni kuchagua maisha
yenye nidhamu katika ulaji.
Maswali ya Msingi ya kujiuliza
·
Nitajuaje kama nahitaji
kufunga?
·
Je nifunge kwa Muda gani?
·
Je ni kila mtu anaweza kufunga?
·
Je kufunga kunaweza ponya aina Fulani ya ugonjwa au hali?
·
Je nitaweza kupungua kiasi gani cha uzito?
·
Upo utofauti gani kati ya kati kufunga kwa kunywa maji pekee na kufunga
kwa kunywa juice pekee?
·
Hali yangu ya umeng’enyaji wa chakula hauwezi kubadilika
wakati na baada ya kufunga na kunisababishia kuongezeka uzito zaidi?
·
Kwa msaada na ushauri zaidi tuma ujumbe kwenye barua pepe; mydailyvalues@yahoo.com or cell;
0767109990
No comments:
Post a Comment