Tuesday, November 27, 2012

KUPUNGUZA UZITO KWAKUTUMIA ASALI NA MDALASINI



Wawezakufurahia vyakula vyote unavyopenda, kuwa na afya nzuri na kupunguza uzito wa mwili ambao hauhitajiki kwa kula chakula chenye nguvu na ladha nzuri, kilichojaa vitu viwili muhimu vya asili ambavyo ni asali na mdalasini.unachohitajika kufanya ni kuhakikisha unavitumia vyote kwa kiasi katika mapishi yako. Vilevile, wataalamu wanasema unaweza kuondoa mabonge ya uvimbe wa nyamanyama nje ya mwili kwa kuanza siku yako kwa kutumia vijiko viwili vya asali iliyochanganywa na kijiko kimoja cha mdalasini ndani ya bilauri ya maji vuguvugu. Rudia mchanganyiko huu kabla ya kulala. Wakati wa kipindi cha baridi kinapokaribia, ambacho kinaambatana na mazoezi machache, kuongeza hivi vitu viwili vya asili katika chakula ni muafaka. Pia kinywaji hiki vuguvugu kimeshahakikishwa na wataalamu wa lishe kwamba hupunguza hamu ya kula pamoja na kuleta joto mwilini.
Tumia Mdalasini na Asali kupunguza uzito.
Jinsi ya kufanya maandalizi ya mchanganyiko huu:
a. Loweka kijiko kimoja cha chai chenye Mdalasini wa unga ndani ya kikombe cha maji ya moto yaliyochemshwa.
b. Koroga kisha funika na Uache kwa muda wa Nusu saa.
c. Baada ya nusu saa chuja kuondoa pumba ya mdalasini kisha weka kijiko kidogo cha Asali.


d. Kunywa asubuhi kabla ya kula kitu chochote nusu saa kabla ya kifungua kinywa, rudia hivi ndani ya wiki kadhaa kwa matokeo bora.

No comments:

Post a Comment


widget