Thursday, August 2, 2012

Papai na Faida Zake kiafya na kimatibabu


Papai hujulikana kwa Lugha nyingine kama Papaya, Paw Paw, Papaw, Tree Melon (botanical name Carica Papaya), lina umbo kama Yai la kuku na langi ya kijani manjano, manjano ama rangi ya chungwa lililoiva vizuri. Papai ni Tunda la mti aina ya mpapai na linaweza kufikia uzito wa kilo mbili na nusu 2.5kg. Kawaida huwa na Radha ya Uchungu Utamu na lina asili ya Ukanda wa Tropiko na maeneo yenye Unyevu mfano Mexico, Amerika ya Kati, Afrika, Asia, Australia nk.
Faida za kiafya za Papai
Sehemu zinayotumika kama Dawa ni Tunda lenyewe, Mbegu, Shina, maganda na Majani yake pia. Unapokuwa sokoni, Gengeni ama Dukani unaweza kununua papai katika hali tofauti tofauti kama majani ya chai, vidonge au Papai lililo bivu, ambalo linaweza kuliwa kama lilivyo, ama kwa kutengenezwa Juice. Huenda unajiuliza ni faida gani hizi za Papai? Sawa tuanze na tunda la papai lina Wingi wa Utomwili, Madini aina ya Folic, Vitamin A, C na E. Pia papai lina kiasi Fulani cha madini ya Calcium, chuma, Riboflavin, Thiamine, na Niacine. Pia Papai linauwingi wa Antioxidant nutrients flavonoids na carotenes, vitamini C, nyingi sana na Vitamin A, na kwa uchache Calories na Sodium. Uweza kjifunza Aina nyingine ya vyakula vyenye Antioxidant Hapa.
Mti wa Papai Papai/Paw paw ina wingi wa  kimeng’enya kwa kimombo-enzymes kijulikanacho kama  papain na chymopapain ambacho husaidia umeng’enyaji wa chakula hasa aina ya Protein tunayokula kuwa Amino Asidi. Utafiti wa karibuni umeonyesha kuwa Amino Asidi Huusika na kila kitu kinachofanywa na Mifumo yetu ya mwili kimsingi mchanyato wa kikemikali mwilini na pia huleta Ujumla wa Afya ya Akili na Mwili. Jinsi tunavyoongezeka umri na ndivyo mwili Huzalisha Vimeng’enya kwa Uchache zaidi ndani ya Tumbo na Kongosho, kitendo ambacho husababisha umeng’enywaji mdogo/ hafifu wa Protein. Na matokeo yake tunapata wingi wa Protein isiyomeng’enywa kwa wingi ambayo husaidia ukuwaji wa vijidudu vya maradhi tumboni. Tunaweza kusema kuwa Kiwango chenye ubora cha Protein ni hasa lazima kwa Afya Zetu na hapo ndipo Kimeng’enya aina ya Papain kipatikanacho kwenye Papai huwa na Faida kubwa Kwetu na kufanya Umuhimu wa Papai Katika maisha ya kila siku.
 Kimeng’enya cha Papain huzalisha kwenye ganda la Papai, na Hii husaidia Papai lisiliwe na wadudu wakati wa kuiva, faida nyingine ya papain ni Kupunguza Uvimbe, Hupunguza Maumivu, hupunguza maumivu ya Magonjwa ya Rheumatoid arthritis, na Osteoarthitis. Kwa Sababu ya wingi wa Antioxidant ndani ya Papai pia huepusha Cholesterol, pia hukinga maradhi ya Atherosclerosis, Strokes, Shinikizo la Moyo, kisukari, Saratani na Magonjwa ya Moyo.  Baada ya kumaliza kutumia Madawa kama Antibiotic kwa Muda ni vyema kula ama kunywa Juisi ya Papai kila siku ili kurejesha Afya ya mwili na Baadhi ya Bacteria wa tumboni ambao husaidia ulinzi na umeng’enyaji chakula walio kufa kwa sababu ya matumizi ya Dawa.
Tafiti zilizofanywa Kuhusu Papai
Stadi zimeonyesha kuwa Papain husaidia pia kupunguza Athari za matibabu ya Kansa, zaidi katika kupunguza maumivu wakati wa kumeza isababishwayo vidonda vya mdomoni baada ya mionzi na dawa, pia hii husaidia kupandisha kinga ya mwili na kusaidia kupambana na Saratani Zipo Bidhaa ambazo zimetengenezwa kwa Papai mfano bidhaa za kampuni ya Rochway ya Australian (kwa taarifa zaidi bofya ama vinjari bapa (rochway.com.au) Kwa kujifunza zaidi juu ya Papai /references na juu ya stadi za karibuni unaweza tazama PubMed Gov.  www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/
Muhtasari wa Hali zinazoweza kurekebishwa na Papai
·         -Muongezeko wa kiwango cha Ubora wa Protien inayohitajika ndani ya Mwili
·         -Huboresha Afya ya mwili na kuufanya kuwa na nguvu ya kutosha kwa muda mrefu
·         -Huchochea uimarishwaji wa Misuli ya mwili
·         -Husaidia Mfumo wa mzunguko wa Damu.
·         -Husaidia Uimarishwaji wa Kinga ya mwili
·         -Husaidia Mfumo wa Umeng’ennyaji wa Chakula na hasa Protein na Huleta Muongezeko wa Uzalishaji wa Vimeng’enya, katika usagaji Chakula.
·         -Husaidia tatizo la Kisukari na Asthma.
·         -Mgonjwa wa Kifua Kikuu akila kwa muda mrefu matunda haya atapona na hutibu kiungulia.
·         -Pia Papai huweza Kutumika kwa nje ya Ngozi kwaajili ya Vidonda, vipele, kansa ya ngozi na vidonda vya moto, Husaidia kupona kwa Haraka vile ambavyo vimekuwa sugu. Kwa kutumia utomvu ama maganda ya papai.
·         -Husaidia Mtu kuzuia kupata Tatizo la mtoto wa Jicho
·         -Kwa sababu uwingi wa Vitamin A, Husaidia watu wanaovuta sigara kuapatwa na tatizo la Emphysema (kujaa Hewa ndani ya Mapafu)
·         -Husaidia kupunguza Uvimbe
·         -Husaidia kupunguza Kichefu chefu na Hali ya kupata choo kigumu / kufunga choo
·         -Huwasaidia Watu walio na Saratani ya chini ya Utumbo mkubwa na aina nyingine za Saratani.
 
UTARATIBU NA MAANDALIZI YA BAADHI YA SEHEMU ZITUMIKAZO KUSAIDIA MATIBABU
*Tumia mbegu ambazo ziko fresh 10-12 kuzitafuna kwa siku kwa Muda wa siku Tano hii hutibu Ini.
*Kausha majani ndani ya nyumba palipo kivuli- haya husaidia kutibu pumu pale inapoanza kubana yachome majani yaliyokauka kisha jifukize kubana kutaisha.
*Papai lilomenywa na kupondwa vizuri hufaa kwa uso na hulainisha ngozi likipakwa kama lotion.
*Mbegu zilizokaushwa ndani ya nyumba na kisha kusangwa na kuwa katika hali ya ungaunga hutibu   Malaria  matumizi Tumia kijiko 1 cha chai changanya na Uji na unywe mara Tatu kutwa kwa siku Tano.
*Mizizi yake ikipondwa na kulowekwa kwenye maji yaliyochemshwa kiasi cha lita mbili na nusu kwa Dakika 15, inasaidia kutibu figo, Kibofu cha mkojo na pia husaidia kuzuia kutapika.
Ningependa kupata Taarifa ya wale hasa wamewahi kutumia ama wanatumia kwa Afya nani sehemu ya mlo wa kila siku ili kuboersha afya zao.
Zingatia : ni muhimu kufuata ushauri wa kitaalamu kabla ya kuanza matibabu ya aina yeyote mbadala kabla ya kumuona daktari ama kufuata taratibu za kitabibu. Ni vyema kuzingatia hivyo kufika kituo cha Afya kwaajili ya vipimo na ushauri wa kitaalamu.


No comments:

Post a Comment


widget