Friday, July 29, 2011

Mning'inio

Mning'inio (Hangover)
Matibabu ya mning’inio ukiwa nyumbani
                                    
          Njia bora sana ya kutibu au ya kuondokana mning’inio uwapo (nyumbani) ni kuacha / kuachana na unywaji pombe. Lakini kwa wale ambao wanapenda pombe vyema kuwa makini na kile kiwango wa ambacho wajua chaweza kukusababishia mning’inio nah ii ni njia mojawapo mtu binafsi waweza kuitambua maana si kila mtu hupata mning’inio kwa kiwango Fulani cha kilevi anachotumia.
Lah! Kama bado unataka kujua dawa ya mning’inio uwapo nyumbani just relux zipo zakutosha hapo ulipo;
Matibabu ya Mning’inio Nyumbani(Hangover)
  • Watu wengi hudhania kuwa kunywa lau glasi au chupa moja asubuhi huondoa mning’inio hii si kweli kabisa, zaidi huongeza kilevi zaidi kwenye mzunguko wa damu!
  • Wala si kikombe cha kahawa kinaweza kukuondolea mning’inio hasha! Ila utakapo kunywa kahawa unaweza pata tatizo jingine la upungufu wa maji mwilini.
  • Njia yenye mafanikio makubwa zaid kutibu/kuondoa mning’inio ni kunywa juisi ya matunda yenye asili ya uchachu chachu hasa yenye uwingi wa vitamini C, Hii wapata fresh ukiwa nyumbani.
  • Kama unapata shida ya maumivu ya kichwa, kuuma sana tumia barafu au (ice bag) kidogo weka  kichwani hii itakupatia nafuu mara kwa muda mfupi.
  • Kuywa maji mengi yakutosha na hii itakufanya uwena maji yakutosha(well hydrated) na kukupunguzia mning’inio.
  • Chai ya Chamomile au peppermint zote zinao uwezo mkubwa wa kukupa nafuu / kuondokana na mning’inio na dalili zake zote, kati ya dawa ambazo wawe pata ukiwa nyumbani hii pia nimojawapo  inayoweza kukupa nafuu haraka sana.
  • Jambo la msingi pia epuka kunywa pombe ukiwa haujala kitu bado, kwanza pata msosi safi baada ya hapo yawezekana kunywa huku pia ukipata vitafunwa Fulani kama nyama choma mishikaki some (snacks) nk.
  • Kujikinga na mning’inio usikupate kunywa pombe katika viwango na mipaka yako na siyo chini ya misukumo yoyote ya kijamii ama marafiki.
  • Red wine, rum and bourbon vinywaji hivi vina rangi nyeusi hivi, unywaji wake unaweza kukuletea athari kubwa yakupata mning’inio.
  • Kabla ya kwenda kulala kunywa maji ya kutosha na hii itakusaidia usipate mning’inio.
  • Pombe  husababisha mwili kupoteza potassium maana mtu hukojoa sana na hii huleta upungufu wa maji mwilini na kufanya kichwa kuuma sana, hivyo kama utakula ndizi itakupatia potassium inayohitajika na kukupunguzia mning’inio.
  • Kama pia unajisikia una kichefu chefu na unatapika, unaweza tafuna tangawizi au katakata vipande vya tangawizi na chemsha kwenye maji kiasi cha birauli kwa dakika kumi kisha changanya na juisi ya chungwa, limao katika viwango sawia na kijiko kimoja au viwili vya asali kwaajili ya ladha. Kisha kunywa na itaondoa mning’inio.
  • Wakati mwingine ukiwa na mning’inio na unahitaji kuondokana nao ni vyema basi kula kitu bila kujali radha mfano wali, au supu ya mbogamboga au plain toust itakufanya ujisikie vizuri na kukuondolea mning’inio.
  • Chukua glasi moja ya maji ya uvuguvugu kisha ongeza humo vijiko viwili vya juisi ya limao na kimoja cha asalis na unywe itakuondilea mning’inio mara moja.
            Pia inawezekana kabisa kuacha sigara na pombe kwa kutumia njia maalumu
                                                                                                          

No comments:

Post a Comment


widget